Pata taarifa kuu
DRC-UN-HAKI

UN yagundua makaburi 38 katika mkoa wa Kasai

Umoja wa Mataifa unasema umegundua makaburi mengine 38 ambayo kwa kiasi kikubwa huenda yakawa ni makaburi mengi ya pamoja kugunduliwa katika mkoa wa Kasai.

Wakazi wa mji wa kasai wakirejea baada ya milio ya risasi kusikika karibu na kambi ya jeshi.
Wakazi wa mji wa kasai wakirejea baada ya milio ya risasi kusikika karibu na kambi ya jeshi. HCR/Celine Schmitt
Matangazo ya kibiashara

Mpaka sasa zaidi ya makaburi 80 ya pamoja yamegunduliwa kwenye mkoa wa Kasai ambapo jumuiya ya kimataifa tayari imeeleza wasiwasi wake kuhusu machafuko yanayoendelea kushuhudiwa kwenye mkoa huo ambao watu zaidi ya elfu 3 wameuawa kwa mujibu wa ripoti ya kanisa katoliki.

Tume ya umoja wa Mataifa nchini DRC MONUSCO awali iliripoti kuwa watu zaidi ya 400 wameuawa toka kuzuka kwa vurugu kwenye mkoa hui huku watu zaidi ya milioni 1 na laki 3 wakidaiwa kukimbia makazi yao.

Umoja wa Mataifa unasema tume yao ya uchunguzi iliyoko nchini DRC imegundua uwepo wa makaburi mengine ya pamoja kwenye mji wa Diboko na Sumbula.

Machafuko kwenye mkoa wa Kasai yalianza mwaka jana wakati kiongozi wa kijadi kwenye eneo hilo Kamwina Nsapu alipouawa na vyombo vya usalama kwenye mpaa wa nchi hiyo na Angola, ambapo alikuwa mkosoaji wa serikali ya rais Joseph Kabila.

Mwezi Februari tume ya MONUSCO iliwashutumu wapiganani wa Kamwina Nsapu kwa kutekeleza makosa ya uhalifu wa kivita ikiwemo kuwasajili watoto kwenye kundi lao lakini ukakosoa namna Serikali inavyotumia nguvu kudhibiti waandamanaji.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.