Pata taarifa kuu
DRC-USALAM-SIASA

Mwenyekiti wa tume ya uchaguzi DRC akosolewa

Mashirika ya kiraia nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, yameeleza wasiwasi wao kuhusu kauli iliyotolewa na mwenyekiti wa tume ya uchaguzi nchini humo Corneille Nangaa Yobeluo, ambaye amesema uchaguzi hautaweza kufanyika kabla ya mwezi Desemba.

Mwenyekiti wa Tume Huru ya Uchaguzi, Corneille Nangaa Yobeluo (kushoto), akitoa hoja zake baada ya kukutana na Mkuu wa ofisi ya MONUSCO, Daniel Ruiz (kulia) mjini Goma.
Mwenyekiti wa Tume Huru ya Uchaguzi, Corneille Nangaa Yobeluo (kushoto), akitoa hoja zake baada ya kukutana na Mkuu wa ofisi ya MONUSCO, Daniel Ruiz (kulia) mjini Goma. MONUSCO/Alain Wandimoyi
Matangazo ya kibiashara

Kauli ya Nangaa imekuja wakati huu ikiwa haijulikani ikiwa uchaguzi mkuu wa nchi hiyo utafanyika kama ilivyokubaliwa kwenye mkataba wa mwezi Desemba mwaka jana.

Kwa matamshi haya ya Nangaa ina maana kuwa huenda uchaguzi mkuu nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo usifanyike kama ulivyopangwa, kwa kile tume inasema ni hali tete ya usalama kwenye eneo la mashariki mwa nchi hiyo na eneo la Kasai.

Mashirika ya kiraia nchini humo yamekosoa matamshi hayo, yakibaini kwamba kauli hiyo inaweza kuchochea uhasama na kuzuka kwa hali ya sintofahamu nchini DRC.

Chini ya makubaliano ya Desemba 31 mwaka jana, rais Joseph Kabila ataongoza Serikali ya mpito na kuhakikisha anaandaa uchaguzi mkuu mwishoni mwa mwaka huu.

Hali ya wasiwasi imeendelea kutanda nchini humo, ambapo bado kunashuhudiwa mvutano kati ya uponzani na chama tawala kikishirikiana na vyama vinavyokiunga mkono.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.