Pata taarifa kuu
LIBYA-USALAMA-HAFTAR

Khalifa Haftar atangaza kuukomboa mji wa Benghazi

Khalifa Haftar anaendesha harakati za kivita mashariki mwa Libya, alitangaza siku ya Jumatano, Julai 5 usiku kwamba wapiganaji wake waliukomboa mji wa Benghazi kutoka makundi ya wanamgambo wa kiislamu na kijihadi.

Wapiganaji wa Khalifa Haftar wakisherehekea ushidi wao wa kuukomboa mji wa Benghazi, Julai 5, 2017.
Wapiganaji wa Khalifa Haftar wakisherehekea ushidi wao wa kuukomboa mji wa Benghazi, Julai 5, 2017. REUTERS/Esam Omran Al-Fetori
Matangazo ya kibiashara

Operesheni hii iliyozinduliwa katika majira ya baridi mwaka 2014, ingelidumu muda wa wiki chache, lakini ilidumu kwa zaidi ya miaka mitatu, wakati ambapo wapiganaji 5,200 wa kiongozi huyo waliuawa. Khalifa Haftar anadai kwamba jeshi lake ni la taifa ya Libya. Ushindi huu wa muda mrefu na mgumu, unampelekea Haftar kuonekana kama mtu mwenye nguvu nchini Libya.

Usiku wa manane siku ya Jumatano wakazi wa Benghazi walikuwa wakisherehekea kukombolewa kwa mji wao. Kwa upande wa baadhi ya vijana wa Benghazi, wamesema tarehe 5 Julai 2017 itabaki kuwa tarehe muhimu katika historia ya Libya, pamoja na kuzuka kwa mapinduzi Februari 17, 2011.

Awali, Khalifa Haftar alitangaza kuwa mji wa pili wa nchi hiyo ulidhibitiwa kutoka kwa makundi ya kigaidi. Siku ya Jumatano, eneo la Souk al-Hout, katikati mwa mji wa Benghazi, ulianguka mikononi mwa wapiganaji wa Khalifa Haftar. Eneo hili ni mihimu kwa sababu harakati na maandamano ya kuung'oa utawala wa aliekua rais wa nchi hiyo Mouammar Kadhafi zilianzia hapo.

Vikosi vya Haftar vinapambana dhidi ya muungano wa magaidi wanaunga mkono kundi la Islamic State, al-Qaeda na Ansar al-Sharia, lakini pia makundi ya kiislamu yasiyo ya kijihadi yanayompinga afisa huyo wa zamani wa ngazi ya juu katika jeshi la zamani la Mouammar Kadhafi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.