Pata taarifa kuu

WHO: Ugonjwa wa Ebola watokomezwa DRC

Maafisa wa afya nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo na Shirika la Afya Duniani wamethibitisha kumalizika kwa janga la virusi vya Ebola Julai 1, 2017.

Kesi nyingi za Ebola zimeonekana katika maeneo ya Likati eneo ambalo ni vigumu kuingia, linalopatikana kwenye mpaka na Jamhuri ya Afrika ya Kati na mikoa mingine miwili ya DRC.
Kesi nyingi za Ebola zimeonekana katika maeneo ya Likati eneo ambalo ni vigumu kuingia, linalopatikana kwenye mpaka na Jamhuri ya Afrika ya Kati na mikoa mingine miwili ya DRC. AFP PHOTO KENZO TRIBOUILLARD
Matangazo ya kibiashara

Tangazo hili linafuatia siku 42 baada ya zoezi la sensa ya kesi ya mwisho ya maambukizikatika mkoa wa Bas Uele, kulitangazwa maambukizi ya virusi vya mtu wa kwanza alieambukizwa, ambaye alipimwa mara mbili bila hata hivyo kupatikana na virusi vya Ebola kwa kipindi cha siku 42.

Hata hivyo kwa hatua za usalama kitengo cha uchunguzi kimewekwa kwa ajili ya kuchunguza virusi hivyo hata kama ugonjwa huo umetangazwa kwamba umekwisha.

Itakumbukwa kwamba ugonjwa wa Ebola uligunduliwa mapema mwezi Mei Kaskazini-Mashariki mwa DRC. Watu wanne walifariki baada ya kuambukiwa virusi vya Ebola na wengine wanne walipona.

Kwa ujumla watu 583 ndio waliambukizwa virusi vya Ebola bila hata hivyo kuonyesha dalili za ugonjwa huo.

Kesi nyingi za Ebola zimeonekana katika maeneo ya Likati eneo ambalo ni vigumu kuingia, linalopatikana kwenye mpaka na Jamhuri ya Afrika ya Kati na mikoa mingine miwili ya DRC.

Ni kwa mara ya DRC kukumbwa na janga la Ebola tangu kugunduliwa kwa virusi vya ugonjwa huo mara ya kwanza mwaka 1976.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.