Pata taarifa kuu
AU-MUGABE

Rais Mugabe auza Ng'ombe wake kufadhili Umoja wa Afrika

Mkutano wa Umoja wa Afrika unamalizika Jumanne jijini Addis Ababa nchini Ethiopia.

Maraia wa Mataifa ya Afrika waliohudhuria mkutano wa 29 wa viongozi wa nchi
Maraia wa Mataifa ya Afrika waliohudhuria mkutano wa 29 wa viongozi wa nchi https://twitter.com/_africanunion?lang=en
Matangazo ya kibiashara

Viongozi wa nchi na serikali wamekuwa wakikutana kuanzia siku ya Jumatatu kujadili maswala mbalimbali yanayolisumbua bara la Afrika.

Mizozo nchini Sudan Kusini, DRC, Jamhuri ya Afrika ya Kati, na kuwepo kwa magaidi nchini Nigeria, Niger na Mali ni masuala ambayo yamekuwa yakijaribu kutafutiwa ufumbuzi wa kudumu.

Mbali na changamoto hizo, Umoja huo umeendele kukabiliwa na changamoto za kifedha kutoka kwa nchi wanachama ambao hawatoi mchango wao kikamilifu.

Katika hatua nyingine, rais wa Zimbabwe Robert Mugabe, ameamua kuuza ng'ombe wake wenye thamani ya Dola Bilioni 1 kufadhili shughuli za Umoja huo.

Rais huyo mkongwe barani Afrika mwenye umri wa miaka 93 ambaye ameongoza nchi yake wake tangu mwaka 1980, alikuwa amepanga kuwaleta ng'ombe hao lakini kutokana na ukosefu wa nafasi katika makao makuu ya Umoja huo, aliamua kuwauza na kuleta fedha.

Mugabe amewaambia viongozi wenzake, kuhakisha kuwa wanafadhili muungano huo kwa fedha zao binafsi kuepuka kutegemea misaada kutoka nchi za Magharibi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.