Pata taarifa kuu
COTE D'IVOIRE-USALAMA

Polisi yafanya msako katika nyumba ya mkuu wa itifaki wa Guillaume Soro

Polisi chini Cote d'Ivoire, iliendesha msako siku ya Jumatatu katika nyumba ya mkuu wa itifaki wa Spika wa Bunge Guillaume Soro, Soul to Soul. Afisaa huyo ambae ni mshirika wa karibu wa Spika la Bunge la Cote d'Ivoire tayari alisikizwa mara kadhaa na polisi katika uchunguzi unaohusiana na silaha zilizogundua hivi karibuni katika mji wa Bouaké.

Katika mji wa Bouake wakati baadhi ya askari walipoasi, Mei 15, 2017.
Katika mji wa Bouake wakati baadhi ya askari walipoasi, Mei 15, 2017. REUTERS/Luc Gnago
Matangazo ya kibiashara

Baada ya ugunduzi wa ghala la silaha katika mji wa Bouake, operesheni kadhaa za misako zimeendeshwa na kitengo cha utafiti cha Polisi. Siku ya Jumatatu mchana polisi waliamua kufanya msako katika nyumba ya afisa huyo

Vyanzo kutoka mahakamani vinabaini kwamba polisi ilikamata simu moja ya mkononi ya mmiliki wa nyumba hiyo iliofanyiwa msako. Kwa sababu tangu mwezi Mei, Soul to Soul amekua akifanyiwa uchunguzi. Wakati baadhi ya askari waliasi, silaha mbalimbali ikiwa ni pamoja na Kalashnikovs na bunduki za aina ya RPG zilikamatwa katika moja ya nyumba ya afisa huyo.

Kwa uchache watu saba walihojiwa. Miongoni mwao, maafisa wa jeshi, amesema Mwendesha mashitaka. Washirika wa karibu wa Guillaume Soro pia walihojiwa na polisi, kwa mujibu wa baadhi ya washirika wa karibu wa Spika wa Bunge la Cote d'Ivoire. Mkuu wa itifaki wa Guillaume Soro alihojiwa mara nne Mkurugenzi na anaweza hivi karibuni kuitishwa na wapelelezi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.