Pata taarifa kuu
UN-DRC

Umoja wa Mataifa waitaka CENI kutangaza kalenda ya Uchaguzi Mkuu

Umoja wa Mataifa unaitaka Tume ya Uchaguzi Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo kuchapisha kalenda ya Uchaguzi Mkuu uliopangwa kufanyika mwishoni wa mwaka huu.

Rais wa DRC  Joseph Kabila
Rais wa DRC Joseph Kabila REUTERS/Tiksa Negeri
Matangazo ya kibiashara

Mjumbe wa Umoja wa Mataifa nchini humo Maman Sidikou, ameitaka Tume hiyo ya Uchaguzi kutangaza kalenda hiyo mara moja kuonesha mipangilio yake.

Hata hivyo, msemaji wa Tume ya Uchaguzi CENI Jean-Pierre Kalamba amemjibu mjumbe huyo wa Umoja wa Mataifa na kumwambia hawezi kutoa maagizo kwa Tume hiyo.

Aidha, amesema hatua ya kuchapishwa kwa kalenda hiyo inaweza tu kuidhinishwa na wabunge ambao sasa hivi wapo mapumzikoni hadi Septemba tarehe 15.

Hadi sasa haijafahamika ikiwa kutakuwa na Uchaguzi kama ilivyopangwa baada ya mwafaka wa kisiasa kupatikana kati ya serikali na upinzani chini ya maaskofu wa Kanisa Katoliki mwezi Desemba mwaka uliopita.

Wapinzani wamekuwa wakisema rais Joseph Kabila ameonesha nia ya kutotaka kuondoka madarakani, madai ambayo kiongozi huyo ameyakanusha na kusema Uchaguzi utafanyika lakini hajasema ni lini.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.