Pata taarifa kuu
JAMHURI YA AFRIKA YA KATI

Mamia wajeruhiwa katika maandamano ya wananchi kupinga mauaji

Mamia ya watu wamejeruhiwa wakiandamana katika miji ya Bria na Bangassou, nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati, wakilaani mauaji ya mara kwa mara yanayoendelea.

Raia wa Jamhuri ya Afrika wakikimbia makwao baada ya mapigano kuzuka
Raia wa Jamhuri ya Afrika wakikimbia makwao baada ya mapigano kuzuka AFP/ISSOUF SANOGO
Matangazo ya kibiashara

Wakiwa wamebeba mabango yaliyoandikiwa maneno ya amani, maridhiano na haki, waandamanaji hao waliandamana pia jijini Bangui na kupiga kambi katika Ikulu ya rais walikoimba wimbo wa taifa wa nchi hiyo.

Mauaji yamekuwa yakiendelea nchini humo tangu mwaka 2013 wakati rais wa zamani Francois Bozize alipoondolewa madarakani kwa nguvu.

Makundi ya waasi Seleka na Anti Balaka yameendelea kupambana nchini humo na hata kukabiliana na vikosi vya usalama na kusababisha vifo vya malefu ya watu na wengine kuyakimbia makwao.

Mwezi uliopita, makubaliano ya kusitisha mapigano yaliafikiwa kati ya makundi ya waasi na serikali nchini Italia lakini imekuwa vigumu kuyatekeleza kutokana na mapigano yanayoendelea.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.