Pata taarifa kuu
SAHEL-UFARANSA-UGAIDI-USALAMA

Macron kusaidia katika vita dhidi ya makundi ya kigaidi katika eno la sahel

Katika mji muu wa Mali, Bamako, wanakutana viongozi wa G5 Sahel, inayoundwa na nchi za Mali, Chad, Niger, Mauritania na Burkina Faso. Mkutano huu unalenga kukamilisha mpango wa kuundwa kwa jeshi la pamoja la askari 5,000 dhidi ya ugaidi.

Ushirikiano kati ya askari wa Mali na askari wa Ufaransa katika operesheni Barkhane.
Ushirikiano kati ya askari wa Mali na askari wa Ufaransa katika operesheni Barkhane. PASCAL GUYOT / AFP
Matangazo ya kibiashara

Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron, mgeni mkuu katika mkutano huu alitoa mapendekezo ya kuunga mkono mpango huu wa wenzake kutoka katika eneo la Saheli.

Katika swala la kijeshi, kwa jumla Ufaransa umeahadi euro milioni nane ifikapo mwishoni mwa 2017 na kusisitiza kipaumbele kwa eneo hili, Rais wa Ufaransa amebaini kwamba msaada unaotolewa kwa Sahel sasa ni sawa na 50% ya bajeti ya ujumla ya ushirikiano kwenye usalama na ulinzi wa Ufaransa duniani.

Msaada kwa maendeleo

Kwa kupambana na umaskini, unaosababishwa na ugaidi, Ufaransa imetoa hadi zake katika swala la maendele.Taasisi ya maendeleo ya Ufaransa (AFD) itatenga milioni 200 hasa kwa nchi G5 katika miaka mitano ijayo, naifikapo majira ya joto, mkurugenzi wa kikanda kwa eneo la Sahel atateuliwa na makao yake makuu yatakuwa katika mjoi wa Ouagadougou.

Hatimaye, Rais alitangaza kuundwa kwa muungano Sahel kwamba itaundwa kuwa misaada mpokeaji wa washirika wote tayari katika maeneo manne: elimu na mafunzo, kilimo, utawala, haki na mapambano dhidi ya mabadiliko ya tabianchi.

Hotuba ya Emmanuel Macron pia inatofautiana na ile ya mtangulizi wake , François Hollande: "sintozungumzia vita kwa sababu wasubiri tu hilo. Kwa kuzungumzia vita, lazima kuwepo na adui anayetambulika, lakini kila sikutunakabiliana na magaidi, majambazi, wauaji ambao tunapaswa kutokomeza, kwa sababu wao wabafanya hivyo kwa lengo la kugawanya watu na dini yenu, ambayo wanaipaka tope kwa kuihusisha na uchochezi wa chuki ", alisisitiza rais Macron.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.