DRC yasema haina tena maambukizi ya Ebola
Serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo imetangaza rasmi kumalizika kwa maambukizi ya ugonjwa hatari wa Ebola nchini humo.
Imechapishwa: Imehaririwa:
Waziri wa afya Oly Ilunga ametoa hakikisho hili baada ya kusema kuwa hakuna kisa chochote cha maambukizi mapya yaliyoshuhudiwa ndani ya siku 42.
Ugonjwa wa Ebola uliripotiwa nchini humo mwezi Mei katika eneo la Kaskazini Mashariki, na kusababisha vifo vya watu wanne na zaidi ya 20 kuambukizwa.
Shirika la afya duniani WHO limeipongeza serikali ya DRC kwa namna ilivyoshughulikia maambukizi haya na kutoa taarifra za mara kwa mara kwa raia wake.
Ebola iliripotiwa kwa mara ya kwanza nchini DRC mwaka 1976 na kusambaa katika maeneo mengine ya dunia.
Ugonjwa huu bado hauna dawa.