Pata taarifa kuu
DRC

Makaburi mapya 10 ya pamoja yagundulika mkoani Kasai

Serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo inasema imegundua makaburi mapya 10 katika mkoa wa Kasai.

Moja ya kaburi katika jimbo la Kasai
Moja ya kaburi katika jimbo la Kasai REUTERS/Aaron Ross
Matangazo ya kibiashara

Kiongozi wa mashtaka katika jeshi la nchi hiyo Jenerali Joseph Ponde, amesema makaburi yamegundulika katika eneo ambalo wanajeshi wa serikali na waasi wamekuwa wakipambana katika siku za hivi karibuni.

Serikali ya DRC imekuwa ikiwashtumu waasi wa Kamuina Nsapu kwa kuwashambulia raia wa kawaida na wanajeshi wa serikali katika mkoa huo.

Wiki iliyopita, Umoja wa Mataifa ulisema raia wa kawaida zaidi ya 2,000 wameuwa katika mkoa huo kwa muda wa miezi mitatu iliyopita.

Aidha, Umoja huo uliituhumu serikali ya Kinshasa kwa kuwafadhili waasi wa Bana Mura kupambana na wale wa Kamwina Nsapu na hivyo kuongeza idadi ya watu waliopoteza maisha nchini humo.

Maelfu ya watu wamekimbilia nchini Angola na wengine katika mikoa mingine nchini humo kutokana na mapigano haya.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.