Pata taarifa kuu
DRC-UN-HAKI ZA BINADAMU

Machafuko ya Grand Kasai kujadiliwa na Tume ya Umoja wa Mataifa ya Haki za Binadamu

Tume ya Umoja wa Mataifa ya Haki za Binadamu inajadili Jumanne hii, June 20 kuhusu machafuko yanayoendelea kushuhudiwa katika jimbo la Grand Kasai nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.

Hotuba ya Afisa mkuu wa Haki za Binadamu huenda ikawa nzito kufuatia takwimu za hivi karibuni, matokeo ya hivi karibuni ya uchunguzi ulioendeshwa na mashirika mbalimbali yasio ya kiserikali.
Hotuba ya Afisa mkuu wa Haki za Binadamu huenda ikawa nzito kufuatia takwimu za hivi karibuni, matokeo ya hivi karibuni ya uchunguzi ulioendeshwa na mashirika mbalimbali yasio ya kiserikali. REUTERS/Denis Balibouse
Matangazo ya kibiashara

Kikao hiki kitazungumzi kuhusi swala la kuundwa kwa tume ya uchunguzi ya kimataifa. Lakini hakuna uhakika wowote katika mpaka sasa. Afisa mkuu wa Haki za Binadamu wa Umoja wa Mataifa, Zeid Ra'ad Zeid Al-Hussein, atajaribu kuzishawishi nchi wanachama wa Umoja huo.

Hotuba ya Afisa mkuu wa Haki za Binadamu huenda ikawa nzito kufuatia takwimu za hivi karibuni, matokeo ya hivi karibuni ya uchunguzi ulioendeshwa na mashirika mbalimbali yasio ya kiserikali. Kwa upande wa Zeid Ra'ad Hussein, kitu muhimu, tunahitaji tume ya uchunguzi ya kimataifa, alioongelea tangu Machi 8.

tume ya uchunguzi ya kimataifa ni muhimu kwa sababu wachunguzi wa Umoja wa Mataifa nchini DR Congo wanaona kazi yao mara kwa mara inakabiliwa na pingamizi nyingi, kulingana na ripoti za siri na ushuhuda. Afisa mkuu wa Haki za Binadamu anataka tume hii itambuliwa kimataifa na kupewa uwezo wa ziada.

Uchunguzi wa pamoja

Serikali ya DR Congo, hata hivyo, imependekeza uchunguzi wa pamoja. Waziri wa Sheria wa DR Congo, Alexis Thambwe Mwamba, amethibitisha hilo siku ya Jumatatu Juni 19. Serikali ya DR Congo itafanya uchunguzi, lakini inataka kusimamia zoezi hili. Umoja wa Mataifa utakuja kusaidia. Huu ni mfumo ambao tayari upo katika kesi mbalimbali, kwa ombi la serikali. Hata bila ya idhini ya kimahakama, kutokana na taarifa za Umoja wa Mataifa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.