Kusikiliza Pakua Podcast
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 04h30 - 05h00 TU
    Uchambuzi na makala 22/05 04h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 05h30 - 06h00 TU
    Uchambuzi na makala 21/05 05h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 15h00 - 16h00 TU
    Uchambuzi na makala 21/05 15h00 GMT
Ili Kufurahia kikamilifu maudhui ya multimedia yetu, unahitaji kuwa na Plugin iliyowekwa kwenye kompyuta yako Ili kuingia, unahitaji kuruhusu cookies zote kwa kuseti vizuri Ili kutembelea mtandao, tovuti ya RFI inaenda sambamba na Internet Explorer 8 na + Firefox 10 na +, Safari 3 na +, Chrome 17 na + nk
Afrika

Mhariri wa gazeti la Tanzania lililofungiwa atishiwa maisha

media Picha sehemy ya magazeti ya Tanzania RFI Kiswahili

Mhariri mkuu wa gazeti moja la Tanzania lililofungiwa na Serikali juma lililopita baada ya kuchapisha habari iliyowahusisha maraisi wa zamani kwenye sakata la mikataba ya madini, amesema toka wakati huo amekuwa akipokea simu za vitisho kutoka kwa watu wasiofahamika.

Wizara ya habari nchini Tanzania tarehe 14 ya mwezi wa 6 ilitangaza kulifungia gazeti la kila wiki la MAWIO kwa muda wa miaka 2 kutokana na hatua yake ya mara kwa mara kuandika habari zinazoikosoa Serikali, ambapo liliandika habari iliyowataja maraisi wastaafu Benjamin Mkapa na Jakaya Kikwete kuhusika kwenye mikataba ya madini.

Uchunguzi wa hivi karibuni ulioagizwa na rais John Pombe Magufuli, umekadiria kuwa kiasi cha dola za Marekani bilioni 84 ambazo ni tozo za kodi zilipotea kutokana na makampuni hayo ya uchimbaji madini yaliyoanza toka mwaka 1998 kukwepa kodi lakini uchunguzi huu haukuwataja popote maraisi hao.

Licha ya onyo lililotolewa na rais Magufuli, gazeti la MAWIO lilichapihs amaoni yaliyotolewa na mbunge wa upinzani Tundu Lissu, ambaye aliliambia bunge kuwa rais Kikwete na rais Mkapa wanahusika pakubwa na utata wa mikataba iliyotiwa saini katika kipindi cha mwaka 1995 hadi 2005 na 2005 hadi 2015 na kwamba walipaswa kuhojiwa na kamati zilizoundwa na rais.

Simon Mkina mhariri wa gazeti hilo ameliambia shirika la habari la Ufaransa la AFP kuwa amekuwa akipokea vitisho vya simu kutoka kwa watu wasiofahamika toka gazeti lao lilipofungiwa.

“Baada ya gazeti kufungiwa, nimepokea takribani simu tatu za vitisho kwa maisha yangu. Niliuliza ninani aliyenipigia lakini alinikatia simu.

“Simu nilizopigia hazikuonesha namba. Kwahivyo nilishindwa kumpigia huyo mtu tena,” alisema muhariri huyo.

Mkina amesema kuwa tayari ametoa taarifa kwa bodi ya gazeti hilo pamoja na jeshi la Polisi ambalo limemjibu kuwa itakuwa vigumu kufanya uchunguzi kwakuwa simu zenyewe hazikuwa na namba.

Timu ya wachunguzi iliyoundwa na rais ilibaini kuwa hasara ambayo Serikali ya Tanzania imeipta ilitokana na makampuni ya kigeni yanayofanya kazi ya uchimbaji madini barani Afrika na amabayo ni ya nne kwa uzalishaji barani humu ilishindwa kutangaza faida miaka yote ya uchimbaji wake nchini Tanzania.

Rais Magufuli aliituhumu kampuni ya Barrick Gold kwa kuiibia nchi yake kupitia njia ya televisheni juma lililopita, lakini alikubali mjadala na mkurugenzi mkuu wa kampuni hiyo John Thornton aliyesafiri kutoka Canada kuja kuona na rais.

Gazeti hili tayari lilikuwa limeshawahi kukutana na zuo wakati wa uchaguzi mkuu uliopita visiwani Zanzibar lakini adhabu hiyo iliondolewa na mahakama.

Mkina amesema gazeti lao limepanga kwenda mahakamani kupinga hatua ya Serikali kulifungua gazeti lao.

Kuhusu mada hiyo hiyo
 
Samahani, mwunganisho na sava umeshindikana