Kusikiliza Pakua Podcast
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 04h30 - 05h00 TU
    Uchambuzi na makala 22/05 04h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 05h30 - 06h00 TU
    Uchambuzi na makala 21/05 05h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 15h00 - 16h00 TU
    Uchambuzi na makala 21/05 15h00 GMT
Ili Kufurahia kikamilifu maudhui ya multimedia yetu, unahitaji kuwa na Plugin iliyowekwa kwenye kompyuta yako Ili kuingia, unahitaji kuruhusu cookies zote kwa kuseti vizuri Ili kutembelea mtandao, tovuti ya RFI inaenda sambamba na Internet Explorer 8 na + Firefox 10 na +, Safari 3 na +, Chrome 17 na + nk
Afrika

13 wauawa katika makabiliano mashariki mwa DRCongo

media Wanajeshi wa jeshi la DRC wakijiandaa kuingia kwenye uwanja wa mapambano Reuters

Mwanajeshi mmoja na wanamgambo 12 wameuawa katika makabiliano yaliyotokea siku ya jumamosi katika jimbo lenye kushuhudia utovu wa usalama Kivu ya kaskazini nchini DRC.

Msemaji wa jeshi la DRC luteni Jules Tshikudi amethibitisha wapiganaji 12 wa Maiamai na afisa wa jeshi la DRC kuuawa katika makabiliano jana jumamosi katika kuwania eneo la Kibasha.

Kundi la Maimai limekuwa likiendesha uasi katika eneo hilo ambapo katika vita ya Congo kati ya mwaka 1998 na 2003 makundi kadhaa yanayomiliki silaha yaliibuka kupambana dhidi ya vikosi vya Uganda au Rwanda lakini baadhi ya makundi hayo hayakusalimisha silaha tangu wakati huo.

Makabiliano ya jumamosi yalizuka baada ya wapiganaji wa Maimai kuvamia na kushambulia kituo cha kijeshi katika eneo la Kibasha ambalo bado linadhibitiwa na serikali na kushuhudia wakazi wakikimbia.

Eneo la Kabasha lipo umbali wa kilomita 24 kusini mwa mji wa Beni, mji ulioshuhudia wimbi a vurugu tangu mwaka 2014 huku takribani 700 wakiuawa wengi wao kuchinjwa hadi kufa.

Kuhusu mada hiyo hiyo
 
Samahani, mwunganisho na sava umeshindikana