Pata taarifa kuu

Polisi yasambaratisha mkutano wa upinzani nchini Mali

Kura ya Maoni ya katiba nchini Mali inatazamiwa kufanyika Julai 9, 2017. Tayari utaratibu wa kura hiyo ya maoni umejulikana. Kadi nyeupe kwa kura ya ndio, na nyingine nyekundu kwa kura ya hapana zitatumia katika uchaguzi huo, kwa mujibu wa taarifa ya Baraza la Mawaziri.

Mji mkuu wa Mali, Bamako, Mei 2016.
Mji mkuu wa Mali, Bamako, Mei 2016. Thomas Imo/Photothek via Getty
Matangazo ya kibiashara

Mageuzi haya yataimarisha mamlaka ya rais. Siku ya Alhamisi asubuhi, maandamano yalifanyika katika mji wa Bamako kupinga musada huo. Maandamano ambayo hayakua yameruhusiwa.

Waandamanaji walikuwa waliomba ruhusa ya kuweza kuandamana kuanziaeneo la Bourse du travail. Lakini serikali ya Mali ilipinga ombi hilo ikieleza kuwa bado kuna hali ya hatari. Hoja hiyo ya serikali hakiwazuia baadhi ya waandamanaji kukusanyika katika eneo moja mjini Bamako.

Vikosi vya usalama vilizuia barabara inayoingia katika majengo ya Bourse du travail, na hivyo kuwa vigumu kwa waandamanaji wengine kujiunga na kundi la kwanza la waandamanaji. Na wakati walijaribu kuandamana, polisi ilitumia nguvu na kuwasambaratisha kutoka majengo ya Bourse du travail. Baada ya makabiliano makali yaliodumu zaidi ya dakika thelathini, waandamanaji waliamua kuitisha mkutano mwingine ndani ya siku mbili zijazo.

Mageuzi haya ya Katiba yalipitishwa na Bunge, kwa kura 111 dhidi ya 35. Ni lazima sasa yapitishwe na kura ya maoni, lakini sehemu moja ya upinzani innakataa kufanyika kwa mageuzi hayo. Itafahamika kwamba marekebisho haya ya katiba yanampa mamlaka mapya rais wa nchi hiyo.

Kulingana na marekebisho hayo, rais wa Mali atakua na uwezo wa kuteua theluthi moja ya maseneta, bila ya kujitetea na pia kuteua Mkuu wa Mahakama ya Katiba. Ni jambo la muhimu sana wakati ambapo inajulikana kwamba Mkuu wa Mahakama ndio anatangaza matokeo ya uchaguzi. Kuwa mtu wake wa karibu ni jambo ambalo linaonekana kuzua hali ya sintofahamu nchini Mali.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.