Kusikiliza Pakua Podcast
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 04h30 - 05h00 TU
    Uchambuzi na makala 25/01 04h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 05h30 - 06h00 TU
    Uchambuzi na makala 25/01 05h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 15h00 - 16h00 TU
    Uchambuzi na makala 25/01 15h00 GMT
Ili Kufurahia kikamilifu maudhui ya multimedia yetu, unahitaji kuwa na Plugin iliyowekwa kwenye kompyuta yako Ili kuingia, unahitaji kuruhusu cookies zote kwa kuseti vizuri Ili kutembelea mtandao, tovuti ya RFI inaenda sambamba na Internet Explorer 8 na + Firefox 10 na +, Safari 3 na +, Chrome 17 na + nk
Afrika

Ufaransa yataka kupelekwa kwa kikosi cha jeshi kutoka Afrika Kusini mwa Sahel

media Ufaransa imeomba Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kusaidia kupelekwa kwa kikosi cha Afrika Magharibi mwa Afrika katika eneo la Sahel kupambana na ugaidi na biashara ya madawa ya kulevya. REUTERS/Lucas Jackson

Siku ya Jumanne Juni 6 Ufaransa iliwasilisha kwa wanachama 15 wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa rasimu ya azimio inayoidhinisha kupelekwa kwa kikosi cha majeshi kutoka Afrika chenye makao yake makuu nchini Mali kupambana dhidi ugaidi na uhalifu uliokithiri.

Ufaransa ina imani kwamba azimio hili, ambalo linasaidia kisheria na kisiasa nguvu ya pamoja inayoitwa G5 Sahel litapitishwa wiki ijayo na litapelekea kuundwa kwa mazingira yenye amani kwa kuhamasisha utekelezaji wa mkataba wa amani uliosainiwa mwaka 2015.

Minusma, kikosi peke cha kulinda amani wa Umoja chaa Mataifa kinachofanya kazi katika mazingira ya kupambana dhidi ya ugaidi kinapaswa kusaidiwa haraka na kikosi cha pamoja kinachoitwa "G5 Sahel".

Kikosi hiki kilichopendekezwa mwezi Machi na marais wa Burkina Faso, Chad, Mali na Niger, na ambacho kitapelekwa kwa kipindi cha awali cha mwaka mmoja kitakua na askari hadi 5,000, ikiwa ni pamoja na polisi na raia wa kawaida.

Kwa mujibu wa azimio liliyoandaliwa na Paris chini ya Sura ya 7, kikosi hiki kitakua na uwezo wote wakutekeleza majukumu yake ya kupambana dhidi ya ugaidi na pia dhidi ya uhalifu uliokithiriri, biashara ya madawa ya kulevya na wahamiaji, biashara ambayo inafadhili kwa kiasi kikubwa makundi ya kijihadi katika eneo hilo.

Bado kuamua jinsi gani kikosi cha G5 Sahel kitaratibu kazi yake katika eneo la Sahel pamoja na vikosi vya Minusma, Barkhane na vikosi vya Mali.

Kuhusu mada hiyo hiyo
 
Samahani, mwunganisho na sava umeshindikana