Pata taarifa kuu
DRC-EU-SIASA

Upinzani DRC waunga mkono hatua ya EU dhidi ya maafisa tisa wa serikali

Mashirika ya kiraia na yale ya kutetea haki za binadamu nchini DRC yameunga mkono hatua ya Umoja wa Ulaya kuwataja na kuwawekea vikwazo maafisa tisa wa serikali kwa kuchelewesha mchakato wa kisiasa nchini humo.

Makao makuu ya manispaa ya jiji la Goma, mkoani Kivu kaskazini.
Makao makuu ya manispaa ya jiji la Goma, mkoani Kivu kaskazini. RFI/Leonora Baumann
Matangazo ya kibiashara

Vyama vya upinzani katika mkoa wa Kivu Kaskazini vimetaka pia maafisa hao wa serikali ya DRC wanaolaumiwa na Umoja wa Ulaya ,wajiuzulu pia madarakani.

"Wamesababisha ukosefu wa usalama! Nasi twaunga mkono uamuzi huo wa Umoja wa Ulaya, waweze kuondoka madarakani kwani wameshindwa, " amesema Neema Vikayilwira, ambae ni mmoja wa viongozi wa upinzani katika mkoa wa Kivu Kaskazini.

Wanasheria wasema ni vema Umoja wa ulaya kuhukumu viongozi wa serikali ulimwenguni , bila upendeleo.

Pia kundi la vijana wa vuguvugu la MK la Moïse Katumbi Chapwe wanasema huenda, vikwazo vitashinikiza viongozi serikalini kuandaa uchaguzi kwa muda uliopangwa.

"Hao ni watu waliofanya kwa makusudi mazima uchaguzi usiandaliwi kwa muda uliowekwa na katiba na ndio maana sisi tunasema vikwazo hivyo vitatusaidia zaidi, " amesema David Paluku Muyisa, kiongozi wa vuguvugu la MK, katika mkoa wai Kivu Kaskazini.

Hata hivyo vyama vya kisiasa vinavyomuunga mkono rais Joseph Kabila Kabange katika mkoa huo vimeshtumu Umoja wa Ulaya kuingilia masuala ya nchi nyingine ambayo iko huru. Vyama hivyo vimemuomba rais Joseph Kabila kuchukua hatua dhidi ya wananchi wa Umoja wa Ulaya.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.