Pata taarifa kuu
MISRI

Waumini 26 wa dhehebu la Coptic wauawa kwa kupigwa risasi nchini Misri

Waumini 26 wa dhehebu la Kikiristo la Coptic wameuawa nchini Misri baada ya watu wasiofahamika waliokuwa wamejihami kwa silaha, kuwavamia na kuwapiga risasi.

Basi lilolokuwa na Wakiristo lilivyoshambuliwa
Basi lilolokuwa na Wakiristo lilivyoshambuliwa Wikipedia
Matangazo ya kibiashara

Watu wengine zaidi ya 20 walijeruhiwa katika tukio hilo. Ripoti zinasema kuwa watu hao walivamia basi lililokuwa na wauamini hao waliokuwa njiani kwenda katika Kanisa lao kongwe katika mkoa wa Minya, katikati ya nchi hiyo.

Gavana wa mkoa huyo Essam el-Bedawi amethibitisha kutokea kwa mauaji hayo na kusema wavamizi hao walitumia silaha nzito dhidi ya waumini hao.

Hakuna kundi lolote lililojitokeza kudai kutekeleza mauaji haya.

Mwezi uliopita, kundi la Islamic State lilishambulia Kanisa la Coptic mjini Alexandria na Tanta na kusababisha vifo vya watu 46.

Mwezi Desemba mwaka uliopita, Wakiristo wa dhehebu hili pia walishambuliwa na kuuawa.

Licha ya rais Abdul Fattah al-Sisi kutangaza miezi mitatu ya hali ya hatari baada ya shambulizi hilo, Wakiristo wameendelea kulengwa nchini humo.

Wakiristo nchini Misri asilimia 10 ya raia wa nchi hiyo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.