Pata taarifa kuu
COTE D'IVOIRE-USALAMA

Idadi ya vifo yaongezeka Cote d'Ivoire baada ya makabiliano

Mji wa Bouake unaendelea kukumbwa na zimwi la machafuko. Baada ya askari walioasi wiki iliyopita, waasi wa zamani ambao hawakuingizwa katika jeshi au polisi wanadai malipo ya malimbikizo yao.

Vikosi vya usalama vya Cote d'Ivoire vyapiga doria katika mji wa Bouake, Jumanne, Mei 23, 2017, baada ya maandamano ya waasi wa zamani waliorejeshwa katika maisha ya kiraia.
Vikosi vya usalama vya Cote d'Ivoire vyapiga doria katika mji wa Bouake, Jumanne, Mei 23, 2017, baada ya maandamano ya waasi wa zamani waliorejeshwa katika maisha ya kiraia. REUTERS/Abdul Fatai
Matangazo ya kibiashara

Takriban waasi wa zamani 6 000 kati yao, kwa mujibu wa hesabu zao wenyewe, wanadai kila milioni Faranga (CFA) milioni 18 (sawa na Euro 27,000 ).

Jumanne asubuhi katika mji wa Bouake, makabiliano ya kutisha yalitokea, wakati ambapo waasi hao wa zamani waliorejeshwa katika maisha ya kiraia walizuia barabara zinazoingia kusini mwa Bouake, mji wa pili kwa ukubwa. Mtu aliyejeruhiwa vibaya katika makabiliano hayo, alifariki siku ya Jumanne mchana katika hospitali, na kutimiza idadi ya waasi wa zamani ambao wamepoteza maisha katika machafuko hayo kufikia wanne.

Siku ya Jumanne jioni hali ya utulivu ilirejea katika mji wa Bouaké. Watu waliripoti kazini na kila mtu alifanya shughuli zake kama kawaida.

Hata hivyo ploisi wameimarisha ulinzi katika maeneo mbalimbali ya mji huo.

Makabiliano makali yalitokea siku ya Jumanne asubuhi kati ya waasi wa zamani waliorejeshwa katika maisha ya kiraia na vikosi vya usalama katika mji wa Bouake.

Wizara ya Mambo ya Ndani imefahamisha kwamba askari watano walijeruhiwa katika makabiliano hayo baada ya mmoja wa waasi hao wa zamani kujaribu kufungua gruneti na kulipuka.

Viongozi wa Cote d'Ivoire wanashtumu waasi wa zamani waliorejeshwa katika maisha ya kiraia kwamba walitumia nguvu na walikua walijihami kwa silaha, madai ambayo yamefutiliwa mbali na waasi hao wa zamani.

Serikali ya Cote d'Ivoire imetoa wito kwa utulivu na kuheshimu sheria wakati mtu anapotetea madai yake.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.