Pata taarifa kuu
WHO-UCHAGUZI-WHO-ADHANOM

Tedros Adhanom achaguliwa Mkurugenzi Mkuu wa WHO

Tedros Adhanom Ghebreyesus, raia wa Ethiopia mwenye umri wa miaka 52, amechaguliwa Jumanne hii Mei 23 Mkurugenzi Mkuu mpya wa Shirika la Afya Dunia, WHO, moja ya mashirika muhimu zaidi ya Umoja wa Mataifa, kwa mujibu wa wanadiplomasia mjini Geneva.

Waziri wa Mambo ya nje wa Ethiopia na Waziri wa Afya Tedros Adhanom, achaguliwa Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Afya Duniani, WHO.
Waziri wa Mambo ya nje wa Ethiopia na Waziri wa Afya Tedros Adhanom, achaguliwa Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Afya Duniani, WHO. AFP PHOTO / ASHRAF SHAZLY
Matangazo ya kibiashara

Aliyekuwa Waziri wa Afya wa Ethiopia alishinda uchaguzi huo dhidi ya wagombea wengine wawili, David Nabarro kutoka Uingereza na Sania Nishtar kutoka Pakistan.

Tedros Adhanom anachukua nafasi ya Bi. Margaret Chan raia wa Canada na Hong kong ambaye amekuwa katika nafasi hiyo kwa karibu miaka 10 sasa.

Akihutubia mkutano wa Afya muda mfupi kabla ya upigwaji kura, Bw Tedros aliahidi kushughulikia dharura zote zitakazojitokeza kwa wakati, haraka na kwa ufanisi. Lakini ameahidi kusimamia haki za masikini, huku akisema kwamba juhudi zote zinapaswa kuelekezwa katika chanjo za afya.

Katika utawala wake, Margareth aliwahi kushutumiwa vikali kutokana na kasi yake ndogo katika kushughulikia mlipuko wa ugonjwa wa Ebola barani Afrika Magharibi. Kitengo hicho kiliwahi kushutumiwa kwa kukosa kuzingatia ishara muhimu za tahadhari juu ya mlipuko hatari wa ugonjwa huo ulioanza mwezi Desemba mwaka 2013.

Itakumbukwa kwamba ugonjwa wa Ebola uliua watu elfu kumi na mmoja katika ukanda huo wa Afrika Magharibi.

Tedros Adhanom Ghebreyesus anajulikana kimataifa kama mtafiti wa malaria, na digirii ya masuala ya afya ya jamii.

Hivi karibuni ametuhumiwa kwa kugubika kesi tatu za ugonjwa wa kipindupindu nchini Ethiopia ingawa wafuasi wake wamekana tuhuma hizo.

 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.