Kusikiliza Pakua Podcast
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 04h30 - 05h00 TU
    Uchambuzi na makala 20/06 04h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 05h30 - 06h00 TU
    Uchambuzi na makala 20/06 05h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 15h00 - 16h00 TU
    Uchambuzi na makala 20/06 15h00 GMT
Ili Kufurahia kikamilifu maudhui ya multimedia yetu, unahitaji kuwa na Plugin iliyowekwa kwenye kompyuta yako Ili kuingia, unahitaji kuruhusu cookies zote kwa kuseti vizuri Ili kutembelea mtandao, tovuti ya RFI inaenda sambamba na Internet Explorer 8 na + Firefox 10 na +, Safari 3 na +, Chrome 17 na + nk
Haraka
Kombe la Dunia 2018: Ureno yaicharaza Morocco 1-0. Timu ya taifa ya Morocco yaaga michuano baada ya kushindwa kwa mara ya pili mfululizo.
Afrika

Transparency International yasema jeshi la Nigeria limekumbatia ufisadi

media Wapiganaji wa kundi la Boko Haram nchini Nigeria REUTERS/Zanah Mustapha

Shirika la Kimataifa la kupambana na ufisadi la Transparency International linasema ufisadi ndani ya jeshi la Nigeria unarudisha nyuma vita dhidi ya kundi la kigaidi la Boko Haram.

Transparency International imesisitiza kuwa hali hii inarudisha nyuma pia juhudi za rais Muhammadu Buhari aliyeingia madarakani mwaka 2015, aliyeahidi kuliangamiza kundi hilo ambalo limesababisha vifo vya maelfu ya watu hasa Kaskazini mwa nchi hiyo.

Shirika hilo linasema kuwa wanajeshi nchini humo wamekuwa wakiingia katika mikataba ya uongo iliyosainiwa nje ya nchini hasa Marekani na Uingereza na kupata idadi kubwa ya fedha.

Mwaka uliopita, serikali nchini humo ilisema kuwa Dola Bilioni 15 ziliibiwa kwa lengo la kununua silaha za kijeshi ambazo hajiziwahi kununuliwa katika vita dhidi ya kundi hili la Boko Haram.

Hata hivyo, madai haya yamekanushwa na jeshi la Nigeria na kusema kuwa madai hayo ya Transparency International si ya kweli.

Meja Jenerali John Enenche, amesema kuwa mengi yamefanywa kuhakikisha kuwa, wanajeshi wanapata mafunzo ya kisasa, kuongeza idadi ya wanajeshi na kununua silaha za kisasa.

Kuhusu mada hiyo hiyo
 
Samahani, mwunganisho na sava umeshindikana