Pata taarifa kuu
COTE D'IVOIRE-USALAMA

Serikali ya Cote d'Ivoire yafikia makubaliano na askari waliogoma

Waziri wa Ulinzi wa Cote d'Ivoire alitangaza siku ya Jumatatu usiku kwenye kituo cha televisheni cha serikali (RTI) kwamba serikali imefikia makubaliano na askari walioasi na kuahidi kulipa madai yao ndani ya siku nne.

askari walioasi katika mji wa Bouaké, Mei 15 2017.
askari walioasi katika mji wa Bouaké, Mei 15 2017. REUTERS/Luc Gnago
Matangazo ya kibiashara

Hata hivyo Waziri huyo hakubainisha utaratibu utakaotumiwa kwa kulipa madai askari hao. Tangazo hilo lililorushwa kwenye kituo cha televisheni cha serikali (RTI) lilidumu dakika zisizozidi 2.

Lakini wazungumzaji wawili wa wanajeshi hao wamesema wamekataa ombi hilo na kuitaka serikali imlipe kila mwanajeshi Faranga CFA milioni tano mpaka saba karibia dola 12,000.

Ni vigumu kusema kuwa wito kwa utilivu uliotolewa na Waziri wa Ulinzi wa Cote d'Ivoire siku ya Jumatatu usiku ulitekelezwa na askari waasi. Katika mji wa pili wa ukubwa nchini humo wa Bouake, hali ya wasiwasi iliendelea kushuhudiwa, na askari walioasi waliendelea kuonekana mitaani, huku risasi ziliendelea kufyatuliwa hewani.

Askari walioasi walikua wakisubiri jana usiku kama malipo wanayoendelea kudai, yaani Faranga CFA milioni 7 zitalipwa kwa pamoja kwa kila askari, kwa mkatomkato, mara moja au kwa kila mwezi.

lakini Waziri wa ulinzi hakubainisha utaratibu utakaotumiwa kwa kuwalipa askai hao waasi

"Makubaliano yalifikiwa kuhusu utaratibu wa kuondokana na mgogoro huu. kwa hiyo tunatoa wito kwa askari walioasi kurejea kambini na kuhakikisha usalam wa wananchi, " waziri wa Ulinzi Alain-Richard Donwahi ametangaza.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.