Pata taarifa kuu
ZAMBIA

Kiongozi wa upinzani nchini Zambia Hakainde Hichilema afutiwa mashtaka ya kuwadharau Polisi

Mahakama jiji Lusaka nchini Zambia, imesema kuwa kesi dhidi ya kiongozi wa upinzani Hakainde Hichilema aliyeshtakiwa kwa makosa ya uhaini itaanza kusikilizwa tarehe 22 mwezi huu.

Kiongozi wa upinzani nchini Zambia Hakainde Hichilema aliyevamia fulana nyekundu baada ya kufutiwa mashtaka Mei 15 2017
Kiongozi wa upinzani nchini Zambia Hakainde Hichilema aliyevamia fulana nyekundu baada ya kufutiwa mashtaka Mei 15 2017 /twitter.com/UPNDZM
Matangazo ya kibiashara

Wakati uo huo, Hakimu Greenwell Malumani amemfutia shtaka lingine kuwa alitoa matamshi ya kuwadhalalisha na kuwadharau maafisa wa Polisi.

Aidha, Malumaini amesema Polisi ambao walikuwa ni mashahidi dhidi ya mwanasiasa huyo, hawakutoa maelezo yanayofanana hivyo hapakuwa na ushahidi wa kumpata na kosa hilo.

Mahakama imewashtumu maafisa wa Polisi kwa kukiuka haki za Hichilema anayefahamika kama HH kwa kumkamata badala ya kufanya uchunguzi wao kwanza.

Mwanasiasa huyu amekuwa akishikiliwa kwa kosa la kuzuia msafara wa rais Edgar Lungu mwezi mmoja uliopita, madai ambayo amekanusha na kusema mashtaka dhidi yake ni ya kisiasa.

 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.