Pata taarifa kuu
NIGERIA-USALAMA

Boko haram yatoa video inayoonesha wasichana waliogoma kurejea makwao

Kundi la wapiganaji la Boko Haram la nchini Nigeria limesambaza video inayowaonesha wasichana wa shule waliogoma kuokolewa katika sehemu ya makubaliano ya serikali ya Nigeria na kundi hilo.

Juma lililopita takribani wasihana 82 waliachiwa huru kurejea kwa wazazi wao
Juma lililopita takribani wasihana 82 waliachiwa huru kurejea kwa wazazi wao REUTERS/Zanah Mustapha
Matangazo ya kibiashara

 

Katika video hiyo ya dakika tatu mwanamke anayejiita Maida Yakubu,anayedaiwa kuwa ni mmoja kati ya wasichana waliotekwa na kundi hilo mnamo April 2014,anaonekana akiwa amevalia hijabu nyeusi na amebeba bunduki.

Akiwa amezungukwa na wanawake wengine watatu waliovalia mavazi kama yake Maida alikiri kutii kundi la Boko Haram, lililogharimu maisha ya zaidi ya watu elfu ishirini tangu lililpoanzisha vurugu dhidi ya serikali ya Nigeria mwaka 2009.

Akijibu swali la mwanaume anayesikika akimuuliza kwa nini hataki kurejea kwa wazazi wake mwanamke huyo alidai kuwa ni kwasababu wazazi wake wanaishi katika mji wa wasio na imani,na kuwataka kuukubali Uislamu.

Juma lililopita takribani wasicha 82 waliotekwa miaka mitatu iliyopita huko Chibok waliachiliwa huru baada ya makubaliano yaliyofikiwa kati ya serikali ya Nigeria na kundi hilo.

Msemaji wa Ikulu Garba Shehu alibainisha kuwa msichana mmoja pekee alikataa kurejea kwa wazazi wake kwa kuwa aliolewa na mmoja wa wapiganaji wa Boko haram.

 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.