Pata taarifa kuu
DRC

Upinzani DRC waahirisha kurejesha nyumbani mwili wa Etienne Tshisekedi

Chama kikuu cha Upinzani cha UDPS nchini  Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo kimeahirisha mpango wa kuurejesha nyumbani mwili wa aliyekuwa kinara wa chama hicho Etienne Tshisekedi.

Mwili wa kiongozi wa upinzani nchini DRC  Etienne Tshisekedi
Mwili wa kiongozi wa upinzani nchini DRC Etienne Tshisekedi EMMANUEL DUNAND / AFP
Matangazo ya kibiashara

Awali, mpango wa kuurejesha nyumbani mwili wa Tshisekedi ulipangwa kufanyika Mei 12.

Katibu mkuu wa chama hicho Jean-Marc Kabund, ameiambia RFI kuwa wameamua kuahirisha mpango huu, ili wapate muda wa kujadiliana na wakuu wa serikali kuhusu taratibu za kutoka jijini Brussels.

Kabund ameongeza kuwa hali ya wasiwasi imeenea katika maeneo jirani na ofisi za chama hicho jijini Kinshasa, ambapo mazingira yaliyopo si ya kuridhisha kutokana na idadi kubwa ya maafisa wa Polisi wanaonekana wakipiga kambi.

Msemaji wa vyama vya kisiasa vinavyomuunga mkono rais Joseph Kabila, Alain Atundu amesema serikali inafuatilia kwa karibu mpango huo, na imejipanga kuhakikisha mazishi ya kinara huyo wa upinzani yanafanyika kwa heshima.

"Viongozi wakuu wa serikali wanafanya kila jitihada kuhakikisha mazishi hayo yanafanyika katika hali yab heshima kulingana na kanuni pia sheria za nchi tangu mwaka 1914 kuhusu maeneo ya kuzika watu, hairuhusiwi kuzika mfu ndani ya mita hamsini na eneo lenye makazi ya watu," alisema Atundu.

 

Naye Naibu Katibu Mkuu wa chama cha UDPS Rubens Mikindo amesema kuahirishwa kwa mpango huo inatoa nafasi ya mazungumzo kuhakikisha kuwa mazishi ya kinara huyo yanafanyika mwezi huu.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.