Kusikiliza Pakua Podcast
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 04h30 - 05h00 TU
    Uchambuzi na makala 21/02 04h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 05h30 - 06h00 TU
    Uchambuzi na makala 21/02 05h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 15h00 - 16h00 TU
    Uchambuzi na makala 21/02 15h00 GMT
Ili Kufurahia kikamilifu maudhui ya multimedia yetu, unahitaji kuwa na Plugin iliyowekwa kwenye kompyuta yako Ili kuingia, unahitaji kuruhusu cookies zote kwa kuseti vizuri Ili kutembelea mtandao, tovuti ya RFI inaenda sambamba na Internet Explorer 8 na + Firefox 10 na +, Safari 3 na +, Chrome 17 na + nk
Afrika

Msafara wa magari ya UN washambuliwa katika mji wa Yogofongo

media Askari wa Kulinda amaniwa umoja wa Mataifa karibu na eneo la PK5 mjini Bangui, mji mkuu Jamhuri ya Afrika ya Kati, wakati wa ziara ya Papa Francis Novemba 10, 2015. REUTERS/Siegfried Modola

Nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati, askari watatu wa kikosi cha Umoja wa Mataifa waliuawa na wanane kujeruhiwa katika shambulizi la Jumatatu 9 Mei kusini mwa nchi hiyo. Askari mmoja hajulikani alipo.

Msafara wa magari ya Kambodia yakilindwa na askari wa Umoja wa mataifa kutoka Morocco ulikua ukitokea Rafai ukielekea Bangassou, miji miwili ilio kwenye mpaka na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, kusini mwa Jamhuri ya Afrika ya Kati. Msafara huyo ulishambuliwa usiku wa Jumatatu katika eneo la Yogofongo, kilomita ishirini kutoka Bangassou. Katika urushianaji risasi kati ya watu wenye silaha na askari wa UN, askari mmoja wa Kambodia aliuawa.

Kwa mujibu wa vyanzo vya Umoja wa Mataifa, shambulizi hilo liliendeshwa na wanamgambo wa Kikristo wa kundi la Anti-Balaka, ambao walikimbilia msituni baada ya shambulio. Baada ya shambulio hilo askari watatu wa Kambodia na mmoja kutoka Morocco walikosekana na kisha miili mitatu ya askari hao kupatikana.Askari wanne bado hajapatikana.

Askari wa UN walengwa na mashambulizi

Katika miezi ya hivi karibuni, eneo la kusini mwa jamhuri ya Afrika ya Kati limeendelea kukabiliwa mapigano kati ya makabila.

Katika mapigano hayo ya kikabila ambayo yanalikumba eneo lote la kusini mashariki mwa nchi, kikosi cha Umoja wa Mataifa nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati, Minusca kimekua kikilengwa.

Kuhusu mada hiyo hiyo
 
Samahani, mwunganisho na sava umeshindikana