Pata taarifa kuu
DRC-USALAMA

Watu 29 wauawa katika Ghasia za wanamgambo Mashariki mwa DRC

Takribani watu 29 wameuawa katika siku tatu za ghasia kati ya makundi yanayomiliki silaha katika eneo lenye utovu wa usalama mashariki mwa DRC,maafisa wamethibitisha.

Wanajeshi wa Serikali ya DRC, wakiwa kwenye misitu ya Beni mashariki mwa DRC
Wanajeshi wa Serikali ya DRC, wakiwa kwenye misitu ya Beni mashariki mwa DRC UN Photo/Sylvain Liechti
Matangazo ya kibiashara

Makundi mawili yanayomiliki silaha yanapambana kudhibiti kijiji cha Bweru katika jimbo la Kivu ya kaskazini,ambalo limekuwa likishuhudia umwagaji damu unaotakana na mapigano ya kikabila.

Kwa mujibu wa kiongozi wa eneo hilo Dieudonne Tshishiku,tangu siku ya jumatano makundi ya wapiganaji wa Mai mai Nyatura yamekabiliana kudhibiti kijiji na kusababisha vifo vya watu 29.

Kiongozi huyo amesema ghasia hizo bado zinaendelea katika kijiji cha Bweru na maeneo ya jirani na kulitaka jeshi la Congo kuingilia kati kukomesha vurugu na kuwarejesha raia waliokimbia makazi yao.

Afisa mmoja wa shirika lisilo la kiserikali amesema pasipo kutaja jina lake kuwa miongoni mwa watu 29 waliouawa ni wapiganaji 11 na kuongeza kuwa raia pia ni miongoni mwa waliouawa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.