Pata taarifa kuu
DRC-UN-MAUAJI

Serikali ya DRC yaonyesha video ya mauaji ya wataalam wawili wa UN

Serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, siku ya Jumatatu Aprili 24 ilionyesha vyombo vya habari video ya mauaji ya wataalam wawili wa Umoja wa Mataifa nchini DRC. Ni picha zinazotisha. Picha ambazo mpaka sasa zilikua mikononi mwa mahakama pekee.

Wataalam wa Umoja wa Mataifa, Zaida Ctalan (picha 2009) na Michael Sharp waliuawa katika mkoa wa Kasai, mwezi Machi 2017.
Wataalam wa Umoja wa Mataifa, Zaida Ctalan (picha 2009) na Michael Sharp waliuawa katika mkoa wa Kasai, mwezi Machi 2017. BERTIL ERICSON, TIMO MUELLER / TT News Agency / AFP
Matangazo ya kibiashara

Raia kutoka Michael Sharp na raia kutoka Sweden Zaida Catalan waliuawa mwezi Machi wakati ambapo walikua wakifanya kuhusu uwezenako wa ukiukwaji wa haki za binadamu uliofanywa katika mkoa wa Kasai ya kati nchini DRC, mkoa uliokumbwa na maandamano ya wafuasi wa kiongozi wa kimila Kamwina Nsapu aliyeuawa mwezi Agosti mwaka jana.

mgogoro huu unaodumu miezi nane sasa umesababisha zaidi ya watu milioni moja kuyahama makazi yao, kwa mujibu wa Umoja wa Mataifa. Kwa upande wa serikali ya DRC, kuonyesha video hii vyombo vya habari na waandishi wa habari wa kigeni ni kutaka kuonyesha machafuko yanayoendeshwa na kundi linalotumia jina la Kamwina Nsapu. "Magaidi", kwa mujibu wa serikali, ambao wanapaswa "kutokomeza".

Picha za kutisha

Katika video hiyo, wataalam wawili wa Umoja wa Mataifa wmekua wakiandamana na kundi la watu katika mashamba. mikono yao haikua imefungwa, wanaonekana wakikusanywa sehemu moja. "Katika lugha ya Tshiluba, lugha inayozungumzwa katika mkoa wa Kasai, watu hawa, waliokua wamezungusha utepe mmwekundu kichwani, walisema wanataka kuwapeleka wachunguzi shemu kunako patikana kaburi la pamoja", msemaji wa polisi alisema siku ya Jumapili.

Katika tukio la pili, watu hao wanaonekana wakiwaomba wataalam kukaa chini. wakisema kwamba mambo yote yatakwenda sawa. Mihael Sharp aliuawa pao hapo. Zaida catalan aliuawa muda mfupi baadaye. wawili miongoni mwa watu hao wnye silaha ambao walikua wakitekeleza amri ya viongozi wao, baadaye walionekana wakikata nywele ya mwanamke mmoja kabla ya kumkata kichwa.

Kwa mujibu wa msemaji wa serikali Lambert Mende, kupitia video ni vigumu kuwatambua wahalifu.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.