Pata taarifa kuu
RFI-AHMED ABBA-CAMEROON

RFI yasikitishwa na hukumu ya Ahmed Abba, wanasheria kukata rufaa

Uongozi wa RFI umeelezea masikitiko yake kufuatia uamuzi wa mahakama ya kijeshi ya Yaoundé, nchini Cameroon, ambayo ilimhukumu Ahmed Abba, mwanahabari wake katika Idhaa ya Hausa nchini Cameroon kifungo cha miaka 10 jela.

Kibonzo kunachoonesha shinikizo la kumwachilia huru Ahmed Abba.
Kibonzo kunachoonesha shinikizo la kumwachilia huru Ahmed Abba. rfi
Matangazo ya kibiashara

Mahakama ya kijeshi ya Yaounde imemuhukua mwaandishi wa habari wa RFI katika Idhaa ya Hausa, Ahmed Abba, miaka 10 jela.

Hii ni adhabu ya chini ikilinganishwa na kosa alilotuhumiwa Ahmed Abba. Ahmed Abba anashtumiwa kosa la kushirikiana na kutetea magaidi. Kosa la "kutetea ugaidi" lilikataliwa kwa sababu ya kukosekana kwa ushahidi wakutosha baada ya RFI kuingilia kati.

Uongozi wa RFI na Shirika la Kimataifa la kutetea haki za Binadamu la Amnesty International wamelaani kifungo hicho ambacho wamesema ni ukiukwaji wa haki.

Mbali na kifungo hicho, Mahakama hiyo imemtaka kulipa faini ya Euro 85,000 kwa kosa la kushirikiana na magaidi, na ikiwa hatalipa faini hiyo, ataongezewa kifungo cha miaka mitano.

Abba alikamatwa mwaka 2015 alipokuwa anawahoji magaidi wa Boko Haram, na kipindi chote cha kesi hiyo alikanusha mashitaka dhidi yake.

Kipindi chote alichoshikiliwa alikuwa anateswa na maafisa wa usalama.

Wakili wake, amesema atakata rufaa dhidi ya hukumu hiyo.

Viongozi wa Mashtaka walitaka ahukumiwe kunyongwa.

Shirika la wabahari wasiokuwa na mipaka RSF sans Frontieres kitengo cha afrika limesema limeguswa na sana na hukumu nzito hiyo katika kosa ambalo halina ushahidi

Wanasheria wa Ahmed Aba wamesema watakata rufaa hii dhidi ya uamuzi huo usiyoeleweka.

Ingawa hakuna ushahidi uliyolitolewa katika kesi hiyo, hukumu hii haieleweki kwa mwandishi wa habari aliyefanya kazi yake.

Mbali na hukumu ya Ahmed Abba, uhuru wa kutoa na kupata habari umewekwa hatarini. RFI imetoa wito kwa minajili ya uhamasishaji kwa wale wote ambao wanatetea uhur wa kutoa na kupata habari kupambana na kutetea haki hii ya msingi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.