Pata taarifa kuu
SOMALIA-NJAA-UKAME

Thomas Wald : Ukame na njaa vyasababisha uharamia kuongezeka Somalia

Hali ya ukame na baa la njaa nchini Somalia, inaelezwa mojawapo ya sababu ya kuongezeka visa vya uharamia katika Pwani ya bahari hindi nchini Somalia.

Wanawake wa Somalia wakikusanya na madumu yao kwa ajili ya kupata maji safi katika kambi ya shirika lisilokua la kiserikali, Aprili 9, 2017.
Wanawake wa Somalia wakikusanya na madumu yao kwa ajili ya kupata maji safi katika kambi ya shirika lisilokua la kiserikali, Aprili 9, 2017. REUTERS/Feisal Omar
Matangazo ya kibiashara

Jenerali wa jeshi la Marekani Thomas Wald Hauser amesema utafiti wao umeonesha kuwa ugumu wa maisha umesbabisha visa hivyo kuongezeka zaidi hasa mwezi uliopita.

Meli na boti za mizigo zimekuwa zikilengwa na maharamia, hivi karibuni walifanikiwa kuwateka mabaharia kutoka India.

Nchi ya Somalia imeendelea kukumbwa na matatizo ya aina mbalimbali ikiwa ni pamoja na vita vya wenyewe kwa wenyewe, hasa mahafuko yanayoendeshwa na kundi la Al Shabab na kusababisha maelfu ya raia kuwa masikini zaidi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.