Pata taarifa kuu
MAREKANI-DJIBUTI-USALAMA

Marekani yaipongeza Ufaransa kwa vita dhidi ya ugaidi Afrika

Waziri wa Ulinzi wa Marekani Jim Mattis ameitaka Ufaransa kuendelea kupambana na ugaidi barani Afrika. Mattis ametoa wito huo baada ya ziara yake nchini Djibouti, eneo ambalo ni la mkakati wa jeshi la Marekani kwa bara la Afrika.

Waziri wa Ulinzi wa Marekani, James Mattis, akisalimu kikosi cha askari wa Ufaransa, Jumapili Aprili 23, 2017, katika Kambi ya Lemonnier, Djibouti.
Waziri wa Ulinzi wa Marekani, James Mattis, akisalimu kikosi cha askari wa Ufaransa, Jumapili Aprili 23, 2017, katika Kambi ya Lemonnier, Djibouti. REUTERS/Jonathan Ernst
Matangazo ya kibiashara

Aidha, amesema kuwa Marekani inaunga mkono Ufaransa katika vita dhidi ya magaidi katika eneo la Sahel hasa nchini Mauritania, Mali, Chad, Niger na Burkina Faso.

Waziri wa Ulinzi wa Marekani James Mattis allimuelezea rais wa Djibouti Ismail Omar Guelleh, wasiwasi wa Marekani kuhusu ujenzi wa kambi ya kwanza ya kijeshi ya China nje ya nchi, karibu na kambi ya Lemonnier ya jeshi la Marekani barani Afrika.

Marekani ina kambi moja peke barani Afrika ambayo imejengwa nchini Djibouti, na ina askari 4,000 kwa mujibu wa Pentagon.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.