Kusikiliza Pakua Podcast
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 04h30 - 05h00 TU
    Uchambuzi na makala 23/05 04h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 05h30 - 06h00 TU
    Uchambuzi na makala 22/05 05h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 15h00 - 16h00 TU
    Uchambuzi na makala 22/05 15h00 GMT
Ili Kufurahia kikamilifu maudhui ya multimedia yetu, unahitaji kuwa na Plugin iliyowekwa kwenye kompyuta yako Ili kuingia, unahitaji kuruhusu cookies zote kwa kuseti vizuri Ili kutembelea mtandao, tovuti ya RFI inaenda sambamba na Internet Explorer 8 na + Firefox 10 na +, Safari 3 na +, Chrome 17 na + nk
Afrika

Intaneti kurejeshwa katika mikoa ya raia wanaozungumza Kiingereza Cameroon

media Rais Cameroon Paul Biya akitoa agizo la kurejeshwa kwa Internet katika maeneo ya watu wanaozungumza Kiingereza Cameroon, baada ya hudum ahiyo kukatwa toka mwezi Januari. AFP PHOTO / REINNIER KAZE

Rais wa Cameroon, Paul Biya, ameagiza siku ya Alhamisi, April 20 kwa makampuni yote yanayotoa huduma za intaneti katika mikoa miwili ya watu wanaozungumza Kiingereza nchini Cameroon kurdudi kufanya kazi.

Katika mikoa hiyo miwili ya kusini magharibi na kaskazini magharibi, intaneti ilikuwa ilikatwa toka mwezi Januari baada ya maandamano ya kudai uhuru zaidi.

Uamuzi wa rais Biya ulitangazwa Alhamisi usiku kwenye masafa ya redio ya taifa. Mikoa hiyo miwili ya watu wengi wanaozungumza Kiingereza nchini Cameroon ilikua haina intaneti toka Januari 17, 2017 baada ya kuzuka maandamani ya kudai uhuru zaidi. Tangu wakati huo, watumiaji wengi wa intaneti na mashirika kadhaa yasiyo ya kiserikaliyalilaani uamuzi huo wa kukatwa kwa intaneti katika mikoa yao.

Katika kutangaza kurejesh intaneti katika mikoa hiyo miwili, serikali ya Cameroon, hata hivyo, ilitoa wito kwa raia kuwa makini na kupinga misimamo na wito wa watu wenye msimamo mkali na maadui wa Jamhuri ya Cameroon."

Kwa upande wake Waziri wa Mawasiliano na msemaji wa serikali Issa Tchiroma Bakary, aliema hakuna sababu leo ya kuendelea kukatwa kwa intaneti katika mikoa hiyo miwili, hata kama serikali haitashindwa kurejelea uamuzi wake ikiwa kutatokea maandamano mengine ya kudai uhuru zaidi.

Kuhusu mada hiyo hiyo
 
Samahani, mwunganisho na sava umeshindikana