Kusikiliza Pakua Podcast
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 04h30 - 05h00 TU
    Uchambuzi na makala 19/04 04h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 05h30 - 06h00 TU
    Uchambuzi na makala 19/04 05h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 15h00 - 16h00 TU
    Uchambuzi na makala 19/04 15h00 GMT
Ili Kufurahia kikamilifu maudhui ya multimedia yetu, unahitaji kuwa na Plugin iliyowekwa kwenye kompyuta yako Ili kuingia, unahitaji kuruhusu cookies zote kwa kuseti vizuri Ili kutembelea mtandao, tovuti ya RFI inaenda sambamba na Internet Explorer 8 na + Firefox 10 na +, Safari 3 na +, Chrome 17 na + nk
Afrika

Vipimo vya DNA vya thibitisha mwindaji aliyepotea aliliwa na mamba

media Mamba. Kelley Miller

Vipimo vya vinasaba DNA vilivyochukuliwa kutoka kwenye tumbo la mamba mmoja aiyeuawa kwa kupigwa risasi nchini Zimbabwe, vimethibitisha kulikuwa na mabaki ya mwili ya mwindaji raia wa Afrika Kusini aliyekuwa amepotea, wamesema wachunguzi walipozungumza na shirika la habari la Uingereza.

Scott Van Zyl aliuawa juma lililopita kwenye kingo za ziwa Limpopo, amesema mkurugenzi wa shirika linalopambana na makosa ya jinai, Sakkie Louwrens.

Kiongozi huyo amesema kuwa Zyl alipotea juma lililopita wakati alipokuwa kwenye safari ya kuwinda.

Kifo chake kimekuwa ni mfululizo wa mtukio ya watu kuuawa kwa kuliwa na mamba nchini Zimbabwe.

Muwindaji huyo ameripotiwa kuwa alikuwa ameenda kuwinda kwenye eneo la mpaka wa nchi hiyo na Zimbabwe akisindikizwa na muongozaji pamoja na mbwa wake.

Taarifa zinasema kuwa walipofika kwenye eneo la tukio kila mtu alienda njia tofauti na mwenzake na kwamba wakati timu ya utafutaji na uokozi ilipoanza kazi ilirejea bila ya Zyl.

Alama za miguu a mwindaji huyo ilibainika kuelekea kwenye kingo za ziwa Limpopo ambako ndiko inaelezwa alikutana na umauti wake.

Maofisa wa wanyamapori kutoka Afrika Kusini walishirikiana na wale wa Zimbabwe kufanikisha utafutaji wa mabaki yake na mamba aliyemla.

Baadae ruhusa ilitolewa kwa mamba huyo kupigwa risasi hadi kufa ambapo miongoni mwa mamba waliouawa mmoja aibainika kuwa na mabaki ya mwili wa Zyl.

Hili ni tukio la nne la mtu kuliwa na mamba kuripotiwa mwaka huu nchini Zimbabwe.
Hata hivyo wanaharakati wa wanyamapori wamekosoa namna ambavyo mamba hao waliuawa buila huruma.

 
Samahani, mwunganisho na sava umeshindikana