Pata taarifa kuu
SOMALIA-AL SHABAB-USALAMA

Al Shabab yaonya wazazi kutowapeleka shule watoto zao

Kundi la Al Shabab limewataka wazazi nchini Somalia kutothubutu kuwapeleka wanao katika shule na vyuo vikuu visivyokuwa vya Kiislam, likidai kwamba elimu ya mfumo wa kimagharibi inapotosha maadili.

Vikosi vya serikali ya Somalia vikipiga doria baada ya gari iliyotegwa bomu kulipuka katika mjini wa Mogadishu, Alhamisi, Januari 22 mwaka 2015.
Vikosi vya serikali ya Somalia vikipiga doria baada ya gari iliyotegwa bomu kulipuka katika mjini wa Mogadishu, Alhamisi, Januari 22 mwaka 2015. REUTERS/Feisal Omar
Matangazo ya kibiashara

Kundi la Al Shabab linadai kwamba elimu ya kimagharibi haihimizi tabia ya maadili mema na kwamba ndio inayowapa motisha raia wa Kisomali kuhamia ulaya.

Kundi la Al Shabab kupitia msemaji wake Ali Mohamoud Rage, katika ukanda wa video uliyorekodiwa dakika i26, amesema “mtu yeyote atakayejihusisha na elimu inayoeneza mila na tamaduni za kigeni atakabiliwa vilivyo”.

Serikali ya Somalia imelishtumu kundi hilo kwa kujaribu kuwanyima watoto wa Kisomalia elimu bora, na kubani kwamba kundi hili linataka kuwaingiza watoto hao kwenye itikadi yao imbaya ya mapigano na mauaji.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.