Pata taarifa kuu
DRC-UVIRA-MAUAJI-AFYA

Mauaji ya daktari Gildo Byamungu yazua hali ya sintofahamu DRC

Raia wa mkoa wa Kivu ya Kusini, hasa wakaazi wa mji wa Uvira wameendelea kueleza masikitiko yao kufuatia mauaji ya daktari wa hospitali ya Uvira, Gildo Byamungu, rafiki wa karibu wa daktari Bingwa Denis Mukwege anayesaidia wanawake wanaonyanyaswa kingono mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.

Bukavu, Aprili 26,2014. Martin Kobler, mkuu wa MONUSCO, alitembelea hopitali ya Panzi inayomilikiwa na daktari Denis Mukwege baada ya kutunukiwa tuzo ya Sakharov 2014 .
Bukavu, Aprili 26,2014. Martin Kobler, mkuu wa MONUSCO, alitembelea hopitali ya Panzi inayomilikiwa na daktari Denis Mukwege baada ya kutunukiwa tuzo ya Sakharov 2014 . MONUSCO/Abel Kavanagh
Matangazo ya kibiashara

Gildo Byamungu, daktari bingwa wa magonjwa ya wanawake katika hospitali ya Uvira, kaskazini mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, alikutwa aliuawa Ijumaa ya wiki iliyopita. Gildo Byamungu alikua rafiki wa karibu wa daktari bingwa maarufu ncini DRC Denis Mukwege, anayejulikana kama "mtu ambaye anasaidia wanawake." Baada ya mauaji ya daktari Byamungu, vyama vya kiraia vimelaani mauaji hayo.

Siku ya Jumanne saa sita mchana katika mji wa Bukavu, raia walitakiwa kutumia kifaa chochote walichonacho kwa kugonga ili kulaani mauaji hayo. Madaktari na wauguzi katika mkoa wa Kivu ya Kusini wametakiwa kufanya mgomo Jumatano hii Aprili 19 wakitaka mwanga utolewe kuhusu mauaji hayo. Wanaomba pia hatua za kuhakikisha usalama wao wakibaini kwamba wamekua wakitishiwa kila mara.

Mpaka sasa haijafahamika mazingira ambao aliuawa daktari Gildo Byamungu wa hospitali ya Kasonga. Tukio hilo lilitokea Ijumaa mjini Uvira. daktari Gilgo Byamungualikuwa nyumbani kwake wakati watu wenye silaha waliingia na kuanza kumfyatulia risasi mara tatuna baadaye kutimka.

Familia ya daktari Byamungu ilijaribu kumsafirisha mjini Bujumbura, nchini Burundi, laini maafisa wa usalama mpaka upande wa Burundi walikataa msafara huo kuingia nchini mwao. Daktari Byamungu alifiriki alipofikishwa kufika hospitali ya Uvira.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.