Pata taarifa kuu
NIGER-USALAMA

Polisi watatu wakamatwa baada ya video ya kutisha kwenye mtandao

Baada ya kifo cha mwanafunzi mmoja siku ya Jumatatu, 10 Aprili, kuna video ambayo imerushwa na kuanza kusambazwa kwenye mitandao ya kijamii, ikionyesha polisi wakimpiga mwanafunzi katika gari yao ndogo. Tukio hilo lilinaswa na polisi wenyewe ambao walirusha video hiyo kwenye mitandao ya kijamii. Watatu kati yao wamekamatwa.

Gereza la Koutoukalé kilometa hamsini kutoka Niamey.
Gereza la Koutoukalé kilometa hamsini kutoka Niamey. AFP
Matangazo ya kibiashara

Video hiyo inayoendelea kusambazwa kwenye mitandao ya kijamii inaonyesha wazi kundi la polisi wakimpiga kikatili mwanafunzi mmoja wa Chuo Kikuu waliokua wakimshikilia. Picha hii imewaghadhabisa raia wengi wa Niger, na kupelekea uongozi wa polisi nchini humo kuanzisha uchunguzi.

"Watatu miongoni mwa polisi hao wametambuliwa kama walihusika katika uhalifu huu, " amesema msemaji wa polisi, Adily Toro. Polisi hao kwamewekwa chini ya ulinzi. Uongozi wa Polisi umelaani kitendo hiki, ukibaini kwamba kamwe hautowalinda wahusika wa kitendo hiki.

Katika taarifa iliyotolewa, Muungano wa walimu na watafiti wa Chuo Kikuu cha Niamey wamelaani na kushtumu mbinu zilizotumiwa na polisi, "Hata wale ambao walikuwa katika madarasa, maktaba, mgahawa, mabweni, misikiti na maeneo mengine hawakutenganishwa wakati wa operesheni hiyo ya polisi ya kuingilia kati, " Muungano huo umebaini.

Kwa upande wa watetezi wa haki za binadamu, tunasema kwa tukilaani. "Mimi nilishtushwa, kwa sababu video hiyo inaonyesha kitendo cha unyama, udhalilishaji, hasa wakati ambapo polisi waliwasili katika eneo la tukio," amelaani Mustafa Kadi Oumani, wa shirika la haki za binadamu la CODDAE.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.