Pata taarifa kuu
NIGERIA

Miaka mitatu baada ya kutekwa na Boko Haram, wasichana wa Chibok hawajapatikana

Miaka mitatu imepita tangu magaidi  wa Boko Haram walipowateka wasichana zaidi ya 200 kutoka shule ya Chibok Kaskazini mwa Nigeria.

Baadhi ya wasichana wa Chibok wakionekana miaka ya hivi karibuni
Baadhi ya wasichana wa Chibok wakionekana miaka ya hivi karibuni AFP
Matangazo ya kibiashara

Serikali ya Nigeria inasema mazungumzo yanaendelea kuhakikisha kuwa wasichana wengine 195 ambao bado wanashikiliwa, wanaachiliwa huru.

Wazazi wa wasichana hao kwa mwaka wa tatu sasa, wanaona kuwa serikali haijafanya juhudi za kutosha kuwaokoa wasichana wao.

Haijafahamika ni wapi waliko wasichana hao, huku ikishukiwa kuwa kuna uwezekano kuwa wamejifichwa katika msitu wa Sambisa.

Jeshi la Nigeria likishirikiana na mataifa mengine kama Cameroon, Niger na Chad wameunda jeshi la pamoja kuwatafuta wasichana hao.

Rais Mohamadu Buhari amekuwa akishtumiwa, na wanaharakati kwa serikali yake kuchukua muda mrefu kuwaokoa wasichana hao.
 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.