Pata taarifa kuu
DRC

Mahakama nchini DRC yamwongezea kifungo mwanasiasa wa upinzani

Mahakama ya rufaa nchini Jamhuri ya Congo, imeongeza mara mbili kifungo cha Waziri wa zamani Jean Claude Muyambo ambaye kwa sasa ni mwanasiasa wa upinzani.

Mwanasiasa wa upinzani Jean Claude Muyambo
Mwanasiasa wa upinzani Jean Claude Muyambo Yutube
Matangazo ya kibiashara

Wakili wake Beaupaul Mupemba amesema mteja wake amehukumiwa jela miaka mitano zaidi baada ya kupatikana na kosa la kuuza nyumba kinyume na sheria.

Mwanasiasa huyo alitarajiwa kuachiliwa huru mwezi Machi, lakini viongozi wa Mashtaka walikwenda katka Mahakama ya rufaa kutaka kifungo hicho kiongezwe.

Inaelezwa kuwa Jengo linalodaiwa kuuzwa kwa utapeli ndilo mwanasiasa wa upinzani na Gavana wa zamani wa jimbo la Katanga, alidaiwa kuuza.

Mwezi Juni mwaka 2016,Katumbi naye alifunguliwa mashitaka kwa madai ya kuuza jengo hilo ambalo inadaiwa sio yake.

Mayumbo ni mmoja wa wanasiasa wa upinzani wanaozuiliwa nchini DRC baada ya kukamatwa katika maandanano ya upinzani jijini Kinshasa mwaka 2015.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.