Pata taarifa kuu
DRCONGO - SIASA

Bruno Tshibala ateuliwa kuwa waziri mkuu mpya wa DRC

Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo Joseph Kabila jana Ijumaa amemteua kiongozi wa upinzani Bruno TShibala kuwa waziri mkuu wa nchi hiyo akiheshimu ahadi aliyoitoa kama sehemu ya kutekeleza makubaliano ya mwezi Disemba mwaka jana kuhusu kugawana madaraka.

Waziri mkuu mpya wa DRC Bruno Tshibala.
Waziri mkuu mpya wa DRC Bruno Tshibala. Capture d'écran vidéo.
Matangazo ya kibiashara

Bruno Tshibala, msemaji wa muungano wa vyamavinavyopinga utawala wa rais Kabila "Rassemblement" anachukua nafasi ya Samy Badibanga, ambaye alijiuzulu nafasi hiyo mapema Ijumaa.

Hata hivyo chama kilichoundwa na kiongozi mkongwe wa upinzani hayati Etienne Tshisekedi,kimejitahidi kuliishi jina lake kwa kupendekeza mwanae Felix Tshisekedi kushika nafasi hiyo.

Tshisekedi ambaye angeongoza baraza la mpito la kusimamia makubaliano ya kuundwa serikali ya mseto kifo chake mwezi Februari kiliugawa upinzani na kujikuta katika mvutano.

Tshibala alipinga shinikizo kutaka mtoto Tshisekedi, Felix Tshisekedi kuchukua uongozi wa chama cha UDPS,hatua iliyosababisha ajiondoe ndani ya chama hicho.
 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.