Pata taarifa kuu
RWANDA - USALAMA

Ghasia zaibuka katika gereza la Gasabo nchini Rwanda

Ghasia zimezuka jana asubuhi katika Gereza la Gasabo mjini Kigali nchini Rwanda. Polisi imefaulu kuzima haraka ghasia hizo ambazo hazikusababisha hasara zozote kwa mujibu wa viongozi wa nchi hiyo. Ghasia na hata maandamano ni jambo lilihaba sana kushuhudiwa nchini Rwanda, nchi ambayo imekuwa ikikosolewa kuhusu kuwanyima haki ya kujieleza wananchi wake.

Jiji la Kigali kutokea paa la jengo la Bunge
Jiji la Kigali kutokea paa la jengo la Bunge @RFI/Stéphanie Aglietti
Matangazo ya kibiashara

Kwa mujibu wa vyombo vya habari nchini Rwanda, huenda kuna uhusiano wa ghasia hizo na tukio la moto lilitokea katika gereza hilo Ijumaa iliopita. Jela hilo la Gasabo linawapokea wafungwa 5.400 wakiwemo waliohukumiwa kuhusika katika mauaji ya Kimbari.

Mapema jana asubuhi mbele ya Gereza la Gasabo, mfanyabiasha mmoja ameeleza kwamba walipata hofu, ambapo mapema jana saa tatu asubuhi wafungwa walivurumisha mawe kutoka ndani ya jela kuelekea maeneo jirani ya jela hilo. Kwa mujibu wa Hillary Sengabo msemaji wa magereza nchini Rwanda, polisi ililazimika kutumia bomu za kutoa machozi ili kuzuma ghasia hizo.

Jana jioni hali ya kwaida ilirejea kushuhudiwa, wakati barabara inayoelekea katika jela hilo ikionekana kusafishwa baada ya kujawa mawe yaliovurumishwa kutoka ndani ya gereza.

Vyombo vya habari nchini humo, vimeendelea kueleza kwamba wafungwa hao walikuwa wakipinga mazingira ya kuzuiliwa kwao baada ya kutokea moto katika gereza hilo siku ya Ijumaa na ambapo watu kadhaa walijeruhiwa.

Msemaji wa magereza Hillary Sengabo amesema uchunguzi umeanzishwa kubaini chanzo cha ghasia hizo, na kuthibitisha kwamba viongozi walitoa uwezo kwa wafungwa walikumbwa na mkasa wa moto, na kwamba wanawasaka wafungwa watovu wanidhwamu katika jela hilo.

Sio mara kwanza tukio kama hilo linatokea nchini Rwanda, tukio la hivi karibuni lilitokea Desemba mwaka jana katika jela la mjini kati na ambapo kila wakati taarifa imekuwa ikitolewa kwamba chanzo chake ni ajali ya kawaida.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.