Kusikiliza Pakua Podcast
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 04h30 - 05h00 TU
    Uchambuzi na makala 25/01 04h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 05h30 - 06h00 TU
    Uchambuzi na makala 25/01 05h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 15h00 - 16h00 TU
    Uchambuzi na makala 25/01 15h00 GMT
Ili Kufurahia kikamilifu maudhui ya multimedia yetu, unahitaji kuwa na Plugin iliyowekwa kwenye kompyuta yako Ili kuingia, unahitaji kuruhusu cookies zote kwa kuseti vizuri Ili kutembelea mtandao, tovuti ya RFI inaenda sambamba na Internet Explorer 8 na + Firefox 10 na +, Safari 3 na +, Chrome 17 na + nk
Afrika

Viongozi wa IGAD wakutana jijini Nairobi kujadili hali ya wakimbizi wa Somalia

media Mkutano wa Mawaziri wa Mambo ya nje kutoka mataifa ya IGAD uliofanyika Ijumaa. tarehe 24 2017 jijini Nairobi IGAD

Viongozi wa nchi za muungano wa IGAD kutoka eneo la pembe ya Afrika, wanakutana siku ya Jumamosi   jijini Nairobi kujadili hali ya wakimbizi wa Somalia wanaondelea kukimbia makwao.

Mkutano huu unatarajiwa kuja na mapendekezo kadhaa na ya muda mrefu kukabiliana na suala hili la wakimbizi ambalo limeendelea kutesa serikali ya Somalia na watu wake.

Hadi sasa raia wa Somalia wapatao Milioni mbili wameyakimbia makwao huku wengi wakiishi nchini Kenya, Ethiopia na nchini Uganda.

Inakadiriwa kuwa wengine zaidi ya Milioni 1 wanaishi nchini humo katika kambi za ndani, katika mazingira magumu.

Umoja wa Mataifa umekuwa ukitoa wito kwa nchi za IGAD hasa Kenya kuendelea kuwapa hifadhi wakimbizi wa Somalia.

Mahakama nchini Kenya mwezi Februari iliamua kuwa mpango wa serikali kuwarudisha nyumbani maelfu ya wakimbizi wanaoshi katika kambi ya Daadad kwa sababu za kiusalama ni kinyume cha katiba ya nchi hiyo.

Mbali na suala la wakimbizi, baa la njaa ni suala lingine ambalo pia litajadiliwa katika mkutano huo.

Suala la usalama pia litapewa nafasi kubwa katika mkutano huo hasa kuwepo kwa kundi la kigaidi la Al Shabab ambalo limeendelea kuzua hali ya wasiwasi katika eneo la Afrika Mashariki.

Mataifa ya IGAD:-Djibouti, Eritrea, Ethiopia, Somalia, Sudan,  Sudan Kusini, Kenya na
Uganda.

Kuhusu mada hiyo hiyo
 
Samahani, mwunganisho na sava umeshindikana