Pata taarifa kuu
MISRI

Rais wa zamani wa Misri Hosni Mubarak aachiliwa huru

Rais wa zamani wa Misri Hosni Mubarak aliyekuwa amepewa kifungo cha maisha jela kwa kuchochea mauaji ya raia wakati wa maandamano ya kumwondoa madarakani mwaka 2011, ameachiliwa huru.

Hosni Mubarak, rais wa zamani wa Misri
Hosni Mubarak, rais wa zamani wa Misri REUTERS/Stringer/Files
Matangazo ya kibiashara

Wakili wake Farid al-Deeb amethibitisha kuachiliwa huru kwa kiongozi huyo wa zamani kutoka Hospitali ya kijeshi ambayo amekuwa akizuiwa kwa miaka sita.

Hatua hii imekuja baada ta Mahakama ya Juu nchini Misri kumwondolea mashtaka ya uchochezi mwezi uliopita na kutangaza kuachiliwa kwake.

Ripoti zinasema kuwa Mubarak baada ya kuachiliwa huru amekwenda nyumbani kwake jijini Cairo.

Baadhi ya raia wa Misri walioshiriki katika maandamano ya kumwondoa madarakani, wamekasirishwa na uamuzi huo kwa kile wanachosema maandamano yao ni kama hayajazaa matunda.

Watu 850 waliuawa nchini Misri katika harakati za siku 18 kushinikiza kujiuzulu kwa Mubarak ambaye alikuwa ameongoza nchi hiyo tangu mwaka 1981 hadi 2011.

 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.