Pata taarifa kuu
DRC-MAUAJI-USALAMA

Askari saba waliohusika katika mauaji Kasai ya Kati wakamatwa

Mahakama ya kijeshi nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo imetangaza kuwa imewakamata wanajeshi saba wanaotuhumiwa uhalifu wa kivita katikati mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, eneo ambalo linakumbwa na ongezeko la machafuko ya wanamgambo kiongozi wa kikabila ambaye aliyeuawa.

wanajeshi saba wanaotuhumiwa uhalifu wa kivita katikati mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, wakamatwa.
wanajeshi saba wanaotuhumiwa uhalifu wa kivita katikati mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, wakamatwa. RFI/Sonia Rolley
Matangazo ya kibiashara

Machafuko hayo yalisababisha vifo vya watu 400, kwa mujibu wa mashirika ya haki za binadamu katika eneo hilo.

Hivi karibuni Umoja wa Mataifa nchini DRC (MONUSCO) ulitangaza kwamba unatiwa "wasiwasi" kutokana na ripoti ya "idadi kubwa ya watu waliouawa" katika siku mbili za mapigano kati ya vikosi vya usalama na wanamgambo wa kiongozi kiroho wa BDK, Kamwina Nsapu, katika taarifa ya siku ya Jumamosi.

Mwezi Februari, video ya kutisha ilioyotengenezwa katika kijiji kimoja cha Kasai ya Kati (katikati mwa DRC) ambayo ilizambazwa kwenye mitandao ya kijamii inaonyesha watu wakivaa sare za jeshi wakiwafyatulia risasi wanakijiji wasio na silaha, au watu waliokua wakirusha mawe na vijiti, kisha wakitoa maneno ya matusi dhidi ya waathirika.

Awali serikali iliitaja video hio kuwa ni ilitengenezwa kwa minajili ya "kupaka tope jeshi lake" kabla ya kuamua kuendesha uchunguzi kwa "tahadhari" dhidi ya madai ya ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu unaoendelea uliohusishwa majeshi ya DRC (FARDC) katika kijiji cha Lomba Mwanza katika mkoa wa Kasai ya Kati.

"Katika uhusiano na video hii, tumewakamata watuhumiwa saba, ambao wote ni askari wa FARDC, na kwa sasa wako kizuizini", miongoni mwao maafisa na askari wa ngazi ya chini, Meja Jenerali Joseph Ponde, mkaguzi Mkuu wa FARDC, alisema katika mkutano na waandishi wa habari.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.