Pata taarifa kuu
DRC-UN-USALAMA

Maafisa 2 wa UN watekwa nyara DRC

Maafisa wawili wa Umoja wa Mataifa wametekwa nyara katika jimbo la Kasai ya Kati, nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, chanzo cha usalama katika umoja wa mataifa kimebaini

Maafisa wa UN na raia wanne wa DRC walitekwa nyara na kupelekwa katika msitu.
Maafisa wa UN na raia wanne wa DRC walitekwa nyara na kupelekwa katika msitu. Getty Images
Matangazo ya kibiashara

Mateka hao ni Michael Sharp kutoka Marekani na Zaida Kikatalani, raia wa Sweden.

Kwa mujibu wa serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, watu hao pamoja na raia wanne wa DRC (waendesha pikipiki za kukodiwa na mkalimani wao) walitekwa nyara na kupelekwa katika msitu.

Mkoa wa Kasai ya kati, wakumbwa na uasi

Vurugu baina ya vikosi vya usalama na wanamgambo zimeendelea kuukumba mkoa wa Kasai ya Kati tangu mwezi Septemba 2016.

Makabiliano hayo tayari yameingia katika mkoa jirani wa Kasai Mashariki na Lomani.

Karibu watu mia nne wameuawa katika machafuko hayo yanayoendelea katika maeneo hayo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.