Kusikiliza Pakua Podcast
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 04h30 - 05h00 TU
    Uchambuzi na makala 15/11 04h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 05h30 - 06h00 TU
    Uchambuzi na makala 15/11 05h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 15h00 - 16h00 TU
    Uchambuzi na makala 15/11 15h00 GMT
Ili Kufurahia kikamilifu maudhui ya multimedia yetu, unahitaji kuwa na Plugin iliyowekwa kwenye kompyuta yako Ili kuingia, unahitaji kuruhusu cookies zote kwa kuseti vizuri Ili kutembelea mtandao, tovuti ya RFI inaenda sambamba na Internet Explorer 8 na + Firefox 10 na +, Safari 3 na +, Chrome 17 na + nk
Afrika

Maporomoko ya taka yagharimu maisha ya zaidi ya watu 30 Ethiopia

media Mlima mkubwa wa taka nchini Ethiopia, nje kidogo ya mji wa Addis Ababa, Machi 12, 2017. AFP

Zaidi ya watu 30 wamepoteza maisha kufuatia maporomoko ya taka kwenye eneo moja kubwa la kumwaga taka nje ya mji mkuu wa Ethiopia Addis Ababa.

Chanzo cha usalama kimesema kuwa watu kadhaa hawajulikani waliko tangu maporomoko hayo yatokee siku ya Jumamosi usiku.

Mashahidi wanasema kuwa watu zaidi ya 150 walikuwa eneo hilo, na inaminiwa kuwa wengi wao wamepoteza maisha.

Eneo hilo limekuwa likitumiwa kutupa taka kutoka kote mjini Addis Ababa kwa zaidi ya miongo mitano.

Inaarifiwa kuwa mabanda mengi ya watu yamefukiwa chini ya taka na watu wamekua wakitafuta vitu vyao.

Serikali nayo imekuwa ikijenga kiwanda cha kwanza barani Afrika, kwa lengo ya kuibadili taka hiyo kuwa nishati karibu na eneo hilo.

Sserikali ina mpango wa kuchoma taka na kuugeuza kuwa umeme. Hata hivyo wa eneo hilo wamekuwa wakisaka eneo hilo kujitafutia riziki.

Kuhusu mada hiyo hiyo
 
Samahani, mwunganisho na sava umeshindikana