Kusikiliza Pakua Podcast
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 04h30 - 05h00 TU
    Uchambuzi na makala 25/01 04h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 05h30 - 06h00 TU
    Uchambuzi na makala 25/01 05h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 15h00 - 16h00 TU
    Uchambuzi na makala 25/01 15h00 GMT
Ili Kufurahia kikamilifu maudhui ya multimedia yetu, unahitaji kuwa na Plugin iliyowekwa kwenye kompyuta yako Ili kuingia, unahitaji kuruhusu cookies zote kwa kuseti vizuri Ili kutembelea mtandao, tovuti ya RFI inaenda sambamba na Internet Explorer 8 na + Firefox 10 na +, Safari 3 na +, Chrome 17 na + nk
Afrika

Polisi ya Afrika Kusini yazima maandamano dhidi ya raia wa kigeni

media Kwa wiki kadhaa, mashambulizi dhidi ya raia kutoka katika Ukanda wa Jangwa la Sahara yameendelea kushuhudiwa Johannesburg. © Getty Images

Alhamisi wiki hii polisi wa Afrika Kusini walifyatua hewani risasi za mpira kuwatawanya waandamanaji walioingia mitaani kwa kile walichosema hawataki raia wa kigeninchini mwao. Maandamano hayo yalifanyika katika mji wa Johannesburg.

Watu watano wamejeruhiwa katika maandamano hayo yaliyofanyika katika eneo la Reiger Park, kitongoji cha mji mkuu wa Afrika Kusini..

Kwa wiki kadhaa, mashambulizi dhidi ya raia kutoka katika Ukanda wa Jangwa la Sahara yameendelea kushuhudiwa Johannesburg.

Maandamano ya Alhamisi wiki hii yalihusu mgao wa makazi ya jamii kwa raia wa kigeni.

Waandamanaji, ambao walichoma matairi na kujaribu kuchoma nyumba ya mwanasiasa wa Afrika Kusini, wanalalamika kuhusu serikali kushindwa kutoa huduma za msingi kama maji na umeme.

Mwezi uliopita, maduka kadhaa na nyumba zinazomilikiwa na wahamiaji Waafrika zilivamiwa karibu na mji wa Pretoria.

Kuhusu mada hiyo hiyo
 
Samahani, mwunganisho na sava umeshindikana