Pata taarifa kuu
AFRIKA KUSINI-WAHAMIAJi

Mamia ya raia wa kigeni wafukuzwa Afrika Kusini

Serikali ya Afrika Kusini imechukua uamuzi wa kuwafukuza raia wa kigeni waishio nchini humo kinyume cha sheria. Watu wakiofukuzwa nchini humo ni kutoka nchi mbalimbali za Afrika hususan raia kadhaa kutoka Nigeria.

Pretoria, Afrika Kusini, Februari 24, 2017: mtu huyu ambaye ameikazwa chini anaonyesha kitambulisho zhake cha uraia wa Afrika Kusini baada ya kuvamiwa wakati wa maandamano dhidi ya wahamiaji.
Pretoria, Afrika Kusini, Februari 24, 2017: mtu huyu ambaye ameikazwa chini anaonyesha kitambulisho zhake cha uraia wa Afrika Kusini baada ya kuvamiwa wakati wa maandamano dhidi ya wahamiaji. REUTERS/ James Oatway
Matangazo ya kibiashara

Vyombo vya habari nchini Nigeria vimekuwa vikiripoti kuwa raia 97 wa Nigeria wanaotuhumiwa kuhusika na uhalifu tofauti walifukuzwa kutoka Afrika Kusini siku ya Jumatatu.

Wizara ya mashauri ya nchi za kigeni nchini Afrika Kusini imethibitisha ripoti kuwa raia kadha wa Nigeria wamefukuzwa kutoka nchini humo.

Raia wengine waliofukuzwa ni pamoja na wale kutoka Pakistan, China, Bangladesh na Somalia.

Msemaji wa wizara hiyi Mayihlome Tshwete anasema kuwa mamia ya watu wasio na vibali walisafirishwa kutoka nchini humo, wengi wao kutoka Jumuiya ya Maendeleo ya nchi za Kusini mwa Afrika (SADC).

Afrika Kusini imekumbwa na ghasia dhidi ya raia wa kigeni na visa vya kuporwa kwa maduka yanayomilikiwa na wahamiaji.

Itafahamika kwamba serikali ya Afrika Kusini huwafukuza watu 30,000 kila mwaka, ambao wanaishi nchini humo kinyume cha sheria au wale wanaohusika na uhalifu tofauti..

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.