Pata taarifa kuu
GAMBIA

Gambia: Bunge laridhia marekebisho ya kipengele cha ukomo wa umri kwenye katiba

Bunge nchini Gambia limeidhinisha kufanyika marekebisho ya katiba kwenye kipengele kinachohusu ukomo wa umri wa kugombea nafasi ya urais, uamuzi uliokuja baada ya rais Adama Barrow, kuhojiwa kuhusu uteuzi wa makamu wake wa rais ambaye alikuwa amevuka umri unaotakiwa kikatiba.

Wafuasi wa rais mpya wa Gambia, wakiweka moja ya bango la kiongozi wa nchi hiyo, Adama Barrow
Wafuasi wa rais mpya wa Gambia, wakiweka moja ya bango la kiongozi wa nchi hiyo, Adama Barrow REUTERS/Afolabi Sotunde
Matangazo ya kibiashara

Mabadiliko haya mapya yamekuja baada ya rais Barrow kukosolewa pakubwa kuhusu uteuzi wa Fatoumata Jallow Tambajang kama makamu wake wa rais huku akijua kuwa alikuwa amezidi umri wa miaka 65.

Kwa mujibu wa marekebisho ya katiba yaliyoanza kufanya kazi mwaka 1997, mtu yeyote mwenye umri wa miaka 65 amezuiwa kuwania nafasi ya juu kwenye Serikali. Katiba hiyo imeongeza kuwa makamu wa rais lazima afikie vigezo vinavyohitajika kteuliwa kwenye nafasi hiyo.

Wiki iliyopita, raia Barrow atahivyo alimtaja mama Tambajang kama waziri aliyepewa mamlaka ya kutathmini kazi za ofisi ya makamu wa rais.

Wachambuzi wa mambo wanasema kuwa uamuzi huu wa bunge kuridhia marekebisho hayo, ni lazima yapasishwe na rais Barrow kabla ya kuwa sheria rasmi, uamuzi ambao sasa utaruhusu Tambajang kuteuliwa rasmi kushika wadhifa huo.

Bunge la nchi hiyo pia, limepitisha marekebisho ambayo sasa yataruhusu majaji wa mahakama kuu kustaafu wakiwa na umri wa miaka 75.

Hata hivyo bunge la nchi hiyo bado kwa sehemu kubwa linatawaliwa na wabunge wa chama cha Yahya Jammeh.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.