Pata taarifa kuu
LIBYA-UHAMIAJI

Zaidi ya miili 70 ya wahamiaji yaokotwa katika pwani ya Libya

Shirika la Msalaba Mwekundu nchini Libya la LRC limesema Jumanne wiki hii kwamba zaidi ya miili 70 ya wahamiaji imegunduliwa katika pwani magharibi mwa mji wa Tripoli, nchini Libya.

Tangu kuanguka kwa utawala wa Muammar Gaddafi, Libya imekuwa ni nchi ya mapokezi kwa wahamiaji haramu wanaoelekea Ulaya.
Tangu kuanguka kwa utawala wa Muammar Gaddafi, Libya imekuwa ni nchi ya mapokezi kwa wahamiaji haramu wanaoelekea Ulaya. © Getty Images
Matangazo ya kibiashara

Wanaume na wanawake ni miongoni mwa waliookotwa wamefariki baada ya boti lililokua likiwasafirisha kuzama.

Kwa mujibu wa CRL, raia wa mkoa huo waligundua boti lililozama katika pwani ya magharibi mwa mji wa Tripoli likiwa na miili kadhaa ya wahamiaji haramu ambao alikua wakijaribu kuingia Ulaya.

Tangu kuanguka kwa utawala wa Muammar Gaddafi, Libya imekuwa ni nchi ya mapokezi kwa wahamiaji haramu wanaoelekea Ulaya.

Idadi kubwa ya wahamiaji waliokutwa wamekufa maji ni kutoka kusini mwa Sahara.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.