Pata taarifa kuu
UN, LIBYA-ICC-HAKI

Umoja wa Mataifa waitaka Libya kumkabidhi Seif al-Islam kwa ICC

Umoja wa Mataifa umeitaka mamlaka ya Libya kumkabidhi mtoto wa Muammar Gaddafi kwa Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu (ICC) kwa mujibu wa ripoti iliyotolewa Jumanne wiki hii.

Seif al-Islam, saa chache baada ya kukamatwa kwake tarehe 19 Novemba 2011, katika mji wa Obari, Libya.
Seif al-Islam, saa chache baada ya kukamatwa kwake tarehe 19 Novemba 2011, katika mji wa Obari, Libya. REUTERS/Ammar El-Darwish
Matangazo ya kibiashara

Seif al-Islam alihukumiwa adhabu ya kifo kwa kuhusika kwake katika ukandamizaji uliosababisha vifo vingi mwaka 2011 nchini Libya.

"Mamlaka ya Libya inapaswa kuhakikisha kuwa imemkabidhi Seif al-Islam kwa Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu (ICC), kwa kuheshimu wajibu wa kimataifa wa Libya," Umoja wa Mataifa umependekeza katika ripoti hiyo.

Kwa mujibu wa ripoti ya tume ya Umoja wa Mataifa nchini Libya (UNSMIL) na ya Ofisi ya Haki za Binadamu (OHCHR) kesi ya Seif al-Islam na maafisa wengine 36 wa utawala wa Kanali Muammar Gaddafi "haikufuatisha viwango vya kimataifa katika suala la kesi inayofuatisha sheria."

Ripoti hiyo "inatambua ugumu wa kuwafikisha mahakamani viongozi wa zamani wa utawala wa Gaddafi katika mazingira ya vita na ubaguzi wa kisiasa."

Hata hivyo, ripoti hiyo aimesisitiza "ukiukwaji mkubwa wa utaratibu wa mara kwa mara, ikiwa ni pamoja na muda mrefu wa kuwekwa kizuizini kwa watuhumiwa," bila kusahau madai ya mateso ambayo hayajafanyiwa uchunguzi sahihi.

Ripoti hiyo inapendekeza serikali ya Libya kuhakikisha kuwa maeneo ya kizuizini kwa watuhumiwa yawe "chini ya udhibiti madhubuti wa serikali" na kwamba madai ya mateso haraka yaweze uchunguzi kwa kina.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.